Zinazobamba

MWIRU KUONDOA MGOGORO WA MIPAKA YA MASHAMBA YA WANANCHI MBARALI.


*Asisitiza wakulima wa mpunga kupata bei elekezi.

*Mbarali kua kituo cha kusambaza chakula shule zote Nchini.

*Azungumzia vurugu za kuvunja Mabasi na vituo vya mwendokasi Dar,asema kuna mkono wa mafisadi.

Na Mussa Augustine.Mbarali Mbeya.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha wakulima(AAFP) Kunje Ngombale Mwiru amesema kuwa endapo Wananchi watakipa ridhaa chama hicho kushika dola atahakikisha anaondoa migogoro wa mipaka ya mashamba ya wakulima wa mpunga Wilayani mbarali Mkoani Mbeya.

Amesema hayo Oktoba 2,2025 katika kata ya Ubaruku Wilayani Mbalali wakati akinadi Ilani ya Chama hicho pamoja nakuwaomba Wananchi kukipigia kura za ndio katika uchaguzi mkuu unaofanyika Oktoba 29 mwaka huu,nakusikitishwa na hatua ya Serikali ya kuwanyang'anya Wakulima hao mashamba yao nakuyaingiza kwenye hifadhi.
"Wazee wa Mbarali wameniambia kuna changamoto kuhusu mipaka ya mashamba ya watu,Serikali iliyopo madarakani inathamini zaidi hifadhi kuliko binadamu hawa, sasa nipende kuwaambia, nchi zote duniani hata kule Ukraine ukioni vita haiishi,ukiona malalamiko hayaishi ujue nyuma ya pazia kuna mtu yupo nao."amesam Mwiru.

Nakuongeza "Na hata hapa Mbarali migogoro hii haitaisha kwasababu kuna mafisadi wadogo wadogo ndani ya Mbarali hii,lakini mafisadi hao nyuma yao kuna watu wanao wasapoti,na ndio maana nimeahidi serikali yangu lazima tulete maheshimiano".
Aidha amesema kuwa akiwa rais wa JMT iataanza kuchukua mafisadi wadogo wadogo,na kuwashughulikia kupitia bwawa la mamba ambalo litachimbwa Ikulu.

"Nimeapa kutoka ndani ya moyo wangu, nikichaguliwa sitakimbilia kwenda Ikulu bali nitakaa miezi miwili niandaliwe bwawa la mamba pale Ikulu ili mafisadi wote wakaliwe na mamba."amesema

Nakuongeza" Mimi Nimetembea nchi nyingi duniani,nimeenda China,nimeenda uturuki wameweka maheshimiano kwenye pesa na mali za umma,China ukitumia vibaya mali za umma unapigwa risasi hadharani,wengine wameanza kusema Ngombale ataweza kweli haya anayo ahidi?..na apa kutoka ndani ya moyo wangu tarehe 29 nipeni muone"amesema 
Katika hatua nyingine amesema kuwa kutokea kwa vurugu za wananchi kuvunja vituo naabasi ya Mwendokasi Jijini Dar es salaam inatokana na wananchi kuchoshwa na adha za usafiri huo wanazozipata.

"Hata hili la kitaifa watu wamevunja mabasi ya Mwendokasi,nchi yoyote malalamiko yakizidi,amani hutoweka, kwasababu kila siku mtu analalamika usafiri shida,maji shida,umeme shida,Kilimo shida lazima nchi inaingia kwenye vurugu."amesema.

Nakusisitiza" Sasa nawaahidi,nimesikia mwenzetu ameteua wengine kwenye kusimamia Mabasi ya mwendokasi,mimi nawambia Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam,nikingia madarakani tarehe 29 watendaji wote wa Serikali nawanyang'anya magari nao waone cha moto kwenye mwendokasi."

Aidha amesema kwamba kwenye mradi wa mwendokasi kuna mkono wa mafisadi,nakwamba mgogoro huo hauwezi kuisha kwasabubu kuna mafisadi ambao wanapata asilimia kumi.
"Nikiwa rais nitamaliza kila kitu haiwezekani ukienda mwendokasi gerezani pale,mama mjamzito,baba mtu mzima anenda pale kwenye kituo cha mwendokasi anakaa zaidi ya saa 3,hakuna huduma yoyote ya kijamii ndani ya kituo,nawatumia Salam tarehe 29 watakiona cha moto."

Akizungumzia kuhusu barabara amesema kuwa miradi hiyo imekua mtaji wa kisiasa hivyo Serikali yake itaweka "Crusher"kwa ajili kuponda mawe na kumwaga zenge kila mahali ili wananchi waweze kupita kila wakati na jambo hilo linawezekana kutokana na nchi ya Tanzania kua na utajiri mkubwa wa milima.

*Power tiller kwa Vijana kuanzia miaka 18.
Amewambia Wananchi wa Mbalali kuwa atatoa power tiller bure  kwa Vijana kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi,huku kila kaya kumi zikipatiwa trekta moja kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo na kupata kipato Cha kuendesha maisha yao.
*Wakina mama wa Mbalimbali kupatiwa mtaji wa biashara.

Aidha amesema kuwa wakina mama ndio walezi wakubwa wa familia,hivyo wanatakiwa kuonewa huruma nakuahidi kua endapo atapewa ridhaa ya kuwa rais wa JMT atahakikisha wanawake kuanzia umri wa miaka 18 watapewa mtaji wa bure wa kuanzia maisha  yao.

"Pesa tunazo, wenzenu wana wadanganya tu pesa hamna pesa hamna,tuna madini,kuna gesi,kuna umeme,tuna kila kitu, kwahiyo wananchi lazima wafurahie matunda ya nchi yao." amesema.
*Kuanzisha mashirika matatu ya umeme yenye ushindani.

Ameendelea kusisitisza kupita ahadi zake kuwa Serikali yake itaanzisha mashirika mengine matatu ya umeme ambayo yatakua na ushindani,tofauti na hivi sasa kuwepo kwa shirika moja la Ugavi wa Umeme (TANESCO) ambalo limeshindwa kuwahudumia Wananchi.

"Umeme una katika katika nitaweka shirika moja la masuala ya gesi,na mashirika mengine mawili kwa ajili ya umeme ili nyinyi wananchi mfaidi matunda ya nchi yenu". amesisitiza 

*Kuhusu maslahi ya walimu Mbarali.

Amesema kuwa amesema kuwa ataweka Mazingira yakinifu ili kuwepo na nyumba bora na huduma za mtandao( internet) ili walimu wanaofundisha Vijijini waweze kufanya kazi zao vizuri.

"Unamchagua mwalimu hapa akafundishe shule huko kijijini hujamuekea mazingira mazuri,Serikali yangu kabla sijachagua walimu kwenda kufundisha vijijini lazima niandae mazingira yakinifu kwa ajili ya mwalimu,nitamjengea nyumba bora,namwekea umeme,na mtandao (internet)aweze kupata mawasiliano na maeneo mengine."amesema 
Nakuongeza" Mbalali ni sehemu tajiri lakini kila ukija Mbalali haibadiliki,ndugu zangu wakulima wa mpunga nichagueni mpate bei elekezi ya mpunga,mpunga mnauza kwa bei ya hasara wapo madalali na vyama vyao wanatembea, unalima mpunga wako baadae unaenda sokoni unarudi na karatasi eti unaambiwa stakabadhi ghalani ndio maana nimesema staki mkulima wangu anyanyaswe katika mazao yake."

Aidha amesema kuwa Serikali yake imepanga Mbalali kua senta ya kuja kuchukua mchele kwa ajili ya kusambaza kwenye shule zote nchi nzima kulisha wanafunzi ambapo kutakua na magari maalumu ya kuja kuchukua vyakula vya wanafunzi.





No comments