Zinazobamba

RAI ASHANGAZWA NA WACHAMBUZI WA SIASA WANAOBEZA AHADI ZA VYAMA VYA SIASA.

Na Mussa Augustine.Mbarali Mbeya.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wakulima AAFP Rashid Rai amewataka wachambuzi wa masuala ya kisiasa Nchini waache kubeza ahadi zinazotolewa na wagombea wa vyama vya siasa kupitia Ilani ya vyama vyao. 

Akizungumza oktoba 2,2025 Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wakati akimnadi Mgombea urais AAFP Kunje Ngombale Mwiru,katibu Mkuu huyo amesema kuwa wachambuzi hao waliofanya uchambuzi kwenye moja ya chombo kikubwa cha habari nchini humo wamekua wakibeza ahadi hizo nakusema hazitekelezeki jambo ambalo ameshangazwa nalo nakusema kuwa ahadi hizo zinatolewa kwa wananchi ili wawe na maamuzi ya kuchagua chama wanachoona kinafaa  kuwaletea maendeleo ya kweli.
Amesema kua moja ya ahadi za AAFP ikiwemo ahadi ya kuweka helkopta kila Wilaya nchi nzima kwa ajili ya kutumika kwa dhalura za majanga kama vile mafuriko inawezekana kutekelezwa kutokana na Serikali kubana matumizi ya kuondoa vyeo vya kisiasa vya wakuu wa Mikoa,Wilaya na Makatibu tarafa,hivyo fedha za kuhudumia viongozi hao zitatumika kuwahudumia wananchi ikiwemo kununua helkopta hizo.

Aidha amesema kwamba kuhusu kujenga barabara za zenge nchi nzima ahadi hiyo inatekelezeka kutokana na Tanzania kujaliwa rasilimali milima nyingi,pamoja na kuwepo kwa viwanda zaidi ya arobaini vya saruji na nondo,hatua ambayo inaondoa gharama za uagizaji wa malighafi kutoka nje ya nchi kama ilivyo kwenye miradi ya kutandaza lami.
Pia amesema kuwa ahadi ya ugawaji wa bodaboda kwa Vijana pamoja na trekta moja kwa kila kaya kumi inawezekana kutokana na kupunguza tozo za kodi ya thamani kwenye bidhaa hizo kutoka nje ya nchi ambako zinauzwa kwa bei ya chini lakini zikisafirishwa kuletwa Nchini Tanzania zinauzwa kwa bei kubwa kutokana na tozo za kodi kua kubwa. 

Hata hivyo Rai amewaomba wananchi kuwa makini na wachambuzi hao ambao wamekua wakipotosha jamii, nakuwasisitiza kuendelea kusikiliza ahadi zinazotolewa na wagombea wote wa vyama vya siasa ili wawe na uwezo wa kupima ni chama kipi kina sera zinazoweza kuwaletea unafuu katika maisha yao.


No comments