DC MAPUNDA AIPONGEZA SERIKALI BAJETI YA KILIMO.
*Aziomba Asasi za kifedha ikiwemo PassTrust kuendelea kuwasaidia Wakulima,Wavuvi na Wafugaji.
Na Mussa Augustine.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es salaam Sixtus Mapunda ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya kilimo kwa kiwango kikubwa kwa miaka minne mfululizo licha ya kuwepo kwa changamoto kubwa ya uzalishaji wa mazao pamoja na masoko.
Amesema hayo leo Oktoba 13,2025 Jijini Dar es salaam kwenye kongamano la miaka 25 Asasi ya kusaidia Sekta binafsi ya kilimo (Private Agricultural Sector Support-Pass trust) kwa lengo la kuwainua wananchi kupitia mnyororo mzima wa thani kwenye masuala ya kilimo,Uvuvi na ufugaji.

"Tuna changamoto kubwa ya uzalishaji,lakini pia tuna changamoto nyingine ya elimu ya kilimo,Uvuvi na ufugaji,tunatambua kwamba hizi ni sekta rasmi sana ambazo jamii ya kitazania inaziona kama sio rasmi sana"Amesema DC Mapunda
DC Mapunda ametoa wito kupitia Pass Trust na taasisi zingine kuongeza kutoa elimu kwa jamii kuona kilimo kama tu kua meneja WA benk,Kilimo ni kikubwa zaidi kwasababu Unapata hapohapo Uliopo na jinsi tunapoelekea huko trend ya dunia inatuonesha hitaji la chakula Duniani linaongezeka mara kwa mara.
Aidha amesema kuwa Jamii itakavyojiweka vizuri katika utunzaji WA mazingingira pamoja na kuongeza mazingira wezeshi ya Serikali kwenye kufanya uwekezaji wa bajeti kubwa,miundombinu ya barabara,reli na ufanisi wa bandari kwenye Sekta ya kilimo,Uvuvi na ufugaji ndani ya muda mfupi Tanzania itakuwa mbali kiuchumi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Pass trust Yohane Kaduma,Mkurugenzi wa Biashara kutoka Asasi hiyo Adam Kamanda amesema kwamba kongamano hilo limehusisha wadau wote wanaoshiriki katika dirisha la Kilimo,Uvuvi na ufugaji katika taasisi za kifefha.
Mkurugenzi wa biashara Pass trust Adam Kamanda."Pass Trust ni taasisi ya fedha ambayo imeanzishwa kwa ubia kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya mfuko wa Waziri mkuu pamoja na Serikali ya Dernmark ikiwa lengo lake kuu ni kuchochea Kilimo biashara ili taasisi za fedha ziweze kuongeza uwekezaji katika Sekta ya kilimo,Uvuvi na mifugo,pamoja na mazao ya misitu."amesema Kamanda
"Nakufafanua kuwa"leo tupo kwenye kongamano hili kubwa ambalo tumelifanya nchi mzima,leo tupo kwenye kilele katika Mkoa wa Dar es salaam ikiunganisha Pwani,Morogoro,Dodoma pamoja na Zanzibar, na tumetoka kufanya kikao kama hiki tukiunganisha Taasisi zote za fedha ambazo zinakopesha Kilimo nchi nzima,kwa hiyo wale wafanyakazi wote kwenye madirisha hayo tumewaunganisha pamoja kama wadau ili kujadili fursa na njia bora ya kukopesha katika Sekta ya Kilimo."
Vilevile amesema kuwa Pass trust imemaliza kufanya kongamano kama hilo katika Mkoa wa Njombe,Arusha Moshi,Kahama,Bukoba nakwamba leo wapo Dar es salaam katika Kanda zao sita.
Amesema kuwa Pass trust hadi sasa katika Sekta ya kilimo imeweza kutoa dhamana zenye thamani ya takribani Tsh.trioni 2.4 katika kipindi cha miaka 25, tangu kuanzishwa kwa Asasi hiyo,nakutumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni imeongeza zaidi bajeti ya kilimo hadi kufikia Tsh. trioni 1.2 bajeti mzima ya Wizara ya kilimo kwawaka 2025/2026.
Meneja uhusiano Coop Bank Khadija Seif akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)kando ya kongamano la miaka 25 la Asasi ya Pass trust lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.



No comments
Post a Comment