Zinazobamba

BABHRA AAHIDI MAKUBWA JiMBONI TEMEKE.

Na.Moshi said

Temeke-Dsm.

Mtia nia wa kinyang'anyiro cha nafasi ya Ubunge wa chama cha Mapinduzi CCM kwa kura za maoni kupitia chama hicho Jasdeep Babhra amesema endapo atapitishwa  na chama chake kuwania Ubunge katika jimbo la Temeke ameahidi kuweka mkazo zaidi katika eneo la Afya na Elimu kwa wananchi wa jimbo hilo.

Babhra ameyasema hayo  katika mkutano wa hadhara wa kujinadi mbele ya  wajumbe wa chama hicho uliofanyika Yombo Makangarawe wilayani Temeke jijini Dar es salaam katika muendelezo wa mikutano ya kujinadi kwa wagombea hao wa nafasi ya Ubunge.

"Nimejenga vyumba nane katika wodi ya wazazi kwa ajiri ya wakina mama kwenda kujifungulia kwa pesa binafsi, nimejenga jiko  katika shule za misingi ambalo linahudumia watoto 1500  bila michango ya wazazi wao , nimejenga maktaba kwa shule ya sekondari kwa ajili ya wanafunzi wetu kwa ajili ya kujisomea"Amesema JASDEEP SINGH

Aidha mtia nia huyo JASDEEP SINGH eliendelea kwa kusema ametoa kadi za bima ya afya kubwa kutoka ufadhili wa ubalozi wa Marekani takribani kaya 77sawa na watu 560 .Sanjari na hilo alipongeza ilani ya chama cha mapinduzi ( CCM)  kwa kuleta dira ya maendeleo ya mwaka 2050 hivyo itapelekea kuleta viongozi waadilifu, wachapa kazi wawazi na kuleta uongozi ambao unaleta maendeleo katika jamii zetu.

Kampeni za kuhitimisha  za kuwapata wagombea watakaokiwalisha chama hicho katika uchaguzi wa mwaka huu zinatarajiwa kumalizika siku ya Jumatatu ya wiki ijayo kabla ya siku ya  Jumanne kupigiwa kura na wajumbe wa chama hicho.



No comments