WANANCHI WAKARIBISHWA TZLPGA SABASABA KUPATA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA GESI YA KUPIKIA MAJUMBANI
Afisa Ufundi na Mafunzo kutoka Chama Cha Waingizaji na Wasambazaji wa gesi ya kupikia Majumbani(TZLPGA)Huruma Msigwa,amesema gesi ni bidhaa hatari kwani inasababisha uharibifu wa mali au kupoteza maisha kutokana na mripuko unaoweza kutokea endapo itatumiwa bila umakini mkubwa.
Msigwa ameyasema hayo Julai 5,2025 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza wa Waandishi wa habari walipotembelea banda la TZLPGA lililopo katika Maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama sabasaba ambayo yameanza Juni 28 na yanafikia tamati Julai 13 Mwaka huu.
"Gesi ni bidhaa ambayo inahitaji umakini hasa wakati wa matumizi,namna ya kuisafirisha,namna gani sahihi ya kutumia vifaa vyake,kwahiyo tunawakaribisha Watanzania waje wapate taarifa sahihi kuhusu Sekta ya gesi ya kupikia Majumbani,Elimu juu ya usalama wake,nakufahamu fursa za uwekezaji katika sekta ya gesi."amesema Msigwa.
Nakuongeza kuwa,Vilevile kufahamu mwelekeo wa sekta ya gesi ya kupikia Majumbani Nchini Tanzania,Afrika na ulimwenguni kote katika nyakati hizi ambapo Dunia inapambana kuhamia katika matumizi ya Nishati safi."
Aidha amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekua ikisisitiza matumizi ya Nishati safi ya kupikia nakuachana na matumizi ya Nishati isiyo salama kama vile kuni na mkaa ambazo zinahatarisha afya na uharibifu wa Mazingira nakusababisha mabadiliko ya Tabianchi yanayopelekea ukame

"Wananchi waje kwenye Banda letu ili watupe maoni na mawazo yao jinsi gani tunaweza tukaboresha utendaji na usalama,katika mkakati huu wa matumizi ya Nishati safi Tanzania ambao umeanza 2024 hadi 2034 ambapo asilimia zisizopungua 80 za Watanzania waweze kupikia Nishati safi ya kupikia,kwani inakadiriwa kwamba gesi hii ya mitungi ina mchango wa asilimia zaidi ya 70 katika kufanikisha mkakati huu."amesema
Aidha amesema kwamba sekta ya gesi inakua kila Mwaka kwa asilimia zisizopungua 10 hadi 15,kwa maana hiyo ni sekta ambayo ina fursa nyingi na inakua kutokana na mwelekeo wa kidunia hasa kuhamia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia.
"Toka tumeanza maonyesho Juni 28,Wananchi wamekua wakija kwenye banda letu,wengi wamekua wakifurahi elimu tunayoitoa kwa maana hii sekta ya LPG hapa Tanzania ni Sekta Changa,ina Wataalamu wachache,vilevile hii bidhaa ni ngeni watu wengi hatujui namna ya kuitumia pamoja na usalama wake,
hatujui dhalura ikitokea tunapambana nayo vipi, kwahiyo watu wengi wamekua wakifurahia elimu ambayo inatolewa,hapa tuna vipeperushi ambavyo vinatoa elimu jinsi ya kutumia ule mtungi mdogo wa kilo 6,mtungi wa kilo 15,na maelekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za matumizi ya gesi."
Halikadhalika Afisa Ufundi na Mafunzo huyo wa TZLPGA amesema kuwa chama hicho kinaendelea kutoa elimu kwa kundi la bodaboda ambao wamekua wakitumiwa kuisafirisha mitungi ya gesi kwa kutumia bodaboda ambapo ni hatari kwa usalama wao na Wananchi wengine.
"Tulifanya utafiti mdogo Dar es salaam, tuligundua kwamba asilimia 50 ya wakazi wa Dar es salaam wana watuma bodaboda kuwachukulia mitungi ya gesi ambapo ni hatari kwani mtungi ukiinamishwa unaweza gesi inavuja na ikitokea chanzo cha moto inaweza kuripuka" amesema Msigwa
Nakufafanua kuwa"Mtungi unatakiwa ubebwe ukiwa umesimamishwa usilazwe kwasabubu pale kwenye valvu ya gesi hakutakiwi kufika kimiminika, kwahiyo ukilaza mtungi kimiminika kitafika kwenye valvu nakusababisha hatari ya gesi kuvuja endapo itakutana na chanzo cha moto inaweza kuripuka."
No comments
Post a Comment