Zinazobamba

TIRA,DSE zatia saini Mkataba wa maridhiano wezeshi ubunifu kifedha.


Na Moshi said.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)  wametia saini Mkataba wa Maridhiano na Soko la hisa la Dar es salaam(DSE ) lengo  kuu ni kuweka mazingira wezeshi ya kuhimiza Maendeleo ya bidhaa bunifu za Kifedha ikiwemo za Bima zinazoweza kuorodheshwa Sokoni,kukuza Elimu ya Kifedha kwa Umma.

Akizungumza leo  Julai 31 jijini  Dar es salaam Kamishna wa TIRA Dkt.Bagayo Saqware wakati wa hafla hiyo  amesema  kuwa  ushirikiano huo ni wa kimkakati ambao utaongeza fursa kwa Kampuni za Bima kupata Mitaji,kupitia Soko la hisa huku ukilinda Maslahi ya walaji na kuhimiza Ufanisi wa Kifedha.Sambamba na hayo amesema makubaliano hayo yatawezesha uboreshaji wa taarifa baina ya TIRA na DSE kwa lengo la kurahisisha Usimamizi na Uchambuzi taarifa ,Uwezeshaji wa kampuni za Bima kuchangia kwenye Soko la Mitaji kwa njia ya kuorodhesha Dhamana zao,Utafiti wa pamoja na Mafunzo ya kitaaluma ili kuongeza uwezo kwa Watumishi wetu pia kusaidia Elimu ya Umma Kuhusu Muhimu wa Bima na Uwekezaji

"Tira inaamini kuwa mafanikio ya Sekta ya Bima hayawezi kutenganishwa na Uimara wa Masoko ya Mitaji kwa pamoja tunaweza Kujenga Mfumo wa Kifedha jumuishi ,imara na wenye manufaa kwa Watanzania wote"Amesema Kamishna.Kwa upande wake  Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la hisa Mkoani Dar es salaam (DSE) Peter Nalitolela amesema makubaliano hayo ni sehemu ya kimkakati ya kuunganisha sekta mbili muhimu  za fedha Nchini Tanzania yaani sekta ya Bima na Masoko ya Mitaji na Dhamana makubaliano ambayo  yatakuwa ni dira ya jinsi Sekta hizo mbili zitakavyofanya kazi  kwa  pamoja ili kuongeza ujumuishaji wa Kifedha kwa Watanzania wote pia kuboresha uwazi na kuchochea Kasi ya mabadiliko na ukuaji wa kiuchumi sambamba na msingi na nguzo za dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Sanjari na hayo amebainisha kuwa itasaidia kuboresha uwezo wa watu na Maendeleo ya Jamii pia Kujenga uchumi imara jumuishi na shindani na Kujenga jukwaa na kubadilishana maarifa  Kati ya Taasisi zetu mbili ili Kujenga Sekta ya Umma na Sekta binafsi zilizo imara.Pia kuandaa kwa pamoja matukio ya kitaaluma ambayo yatawakutanisha wadau wote Muhimu kutoka Sekta ya Bima,Masoko ya Mitaji,wawekezaji,hii itasaidia Kati uimarishaji wa Sekta za kimageuzi na kuendelea mbinu Bora za Usimamizi wa hatari na uwazi wa  taarifa itasaidia kuchangia Kujenga uchumi-jumla tulivu na unaotabirika.

No comments