Zinazobamba

SERIKALI YA DKT. SAMIA YAPEWA HONGERA KWA JITIHADA ZA KUELIMISHA WASICHANA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti wa Bodi ya GPE Duniani, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa mafanikio makubwa katika sekta ya elimu, ikiwemo ongezeko la ufaulu na idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu.

Kikwete ameyasema hayo Julai 14, 2025 Jijini Dar es salaam katika Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam, wakati Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), Malala Fund na Global Partnership for Education (GPE), walipotembelea Shule hiyo.Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. QS Omari Kipanga amesema mabadiliko ya mitaala yamejenga mazingira salama na jumuishi kwa wanafunzi wote, hasa wasichana na wenye mahitaji maalum huku akisisitiza kuwa teknolojia ya kidijitali na matumizi ya AI sasa ni sehemu ya mitaala, na serikali inaendelea kuhimiza ushiriki wa wasichana kwenye masomo ya TEHAMA na STEM.Kwa upande wake Malala Yousafzai, Mwanzilishi wa Malala Fund, amesifu juhudi za Tanzania katika kuwawezesha wasichana kupata elimu, huku akitoa wito kwa jamii kuungana kuhakikisha wasichana hawakatishi masomo yao.



No comments