Zinazobamba

MRADI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME KILOLENI MKOANI TABORA UMEFIKIA ASILIMIA 80 -MD TWANGE


Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa kituo cha kupoza umeme cha Kiloleni kilichopo Mkoani Tabora ambapo amesema Mradi huo  umefikia asilimia 80.

Bw. Lazaro Twange  amefanya ziara hiyo  Julai 4 2025 akiwa ameongozana na Meneja wa Kanda ya Magharibi Mhandisi. Richard Swai pamoja na Meneja wa Mkoa wa Tabora Mhandisi Amina  Ng'imba ambapo amesema amerishishwa na kasi ya utekelezaji wa  mradi huo ambao hadi kukamilika kwake unatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 14.6.

Amesema Kituo cha kupoza umeme cha Tabora mjini kilichopo eneo la kiloleni Manispaa ya Tabora  ni miongoni mwa vituo tisa vya kupoza umeme hapa nchini vinavyofanyiwa marekebisho ikiwemo uboreshaji wa miundombinu kupitia mradi wa TT group ili kuzalisha umeme wa uhakika na kuwaondolea adha wananchi.Katika ziara hiyo  Bw. Twange pia alipata nafasi ya kuzungumza na wafanyakazi wa TANESCO Mkoani Tabora ambapo amewapongeza  Kwa utendaji wa kazi mzuri huku akiwasisitiza  kuendelea kufanya kazi Kwa weledi, upendo na mshikamano.



No comments