KAMISHNA LYMO ASIFIA MAFANIKIO YA VITA YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI.
Na Mwandishi Wetu.
Akizungumza katika banda la DCEA, Kamishna wa Mamlaka hiyo, Aretas Lyimo, amesema ushiriki wa taasisi hiyo katika maonesho hayo ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuelimisha jamii kuhusu aina mbalimbali za dawa za kulevya,athari zake kwa mtumiaji na jamii kwa ujumla, pamoja na hatua kali za kisheria zinazochukuliwa dhidi ya wahusika.
“Tupo hapa ili wananchi wapate elimu ya kutosha kuhusu dawa za kulevya na aina zake,madhara yake,pi wajue kwamba sheria iko wazi kuhusu mtu yeyote atakayekamatwa akiwa anazimiliki, kuzisambaza au kuzitumia,” amesema Kamishna Lyimo.
Nakuongeza kuwa "kwa sasa DCEA iko katika oparesheni maalum inayoendeshwa katika shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kwa lengo la kutoa elimu ya kinga kwa vijana."
Akizungumzia hali ya waathirika wa dawa za kulevya,Kamishna Lyimo ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita inatoa huduma za matibabu bila malipo kwa wote walioathirika,ili kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida na kushiriki katika shughuli za maendeleo ya taifa.
“Hii ni hatua muhimu ya huruma na uwekezaji wa serikali kwa watu wake. Tunataka kila Mtanzania awe na afya njema na asiwe mateka wa uraibu wa dawa hizi hatari,”amebainisha Kamishna huyo wa DCEA.
Pia ameeleza kuwa kutokana na oparesheni mbalimbali zinazoendelea kufanyika nchi nzima, hali ya matumizi na upatikanaji wa dawa za kulevya inazidi kuimarika. Dawa za kulevya hatari kama vile heroin na cocaine zimepungua kwa kiasi kikubwa nchini.
Maonesho ya Saba Saba mwaka huu yanaendelea hadi Julai 13, na DCEA inatoa wito kwa wananchi wote kutembelea banda lao ili kupata elimu ya kina juu ya namna ya kujikinga na madhara ya dawa za kulevya na kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya janga hili ambalo lina athiri nguvu ya Taifa.
No comments
Post a Comment