Zinazobamba

Mbeto :OMO simama kwa miguu yako muache Maalim Seif apumzike peponi.


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi  kimemtaka Mwenyekiti  wa ACT Wazalendo  ,Othman Masoud  Othman,  kuwaeleza Wazanzibari atawafanyia mambo  gani  ambayo hayajatekelezwa na Rais  Dk Hussein  Ali Mwinyi pia  amwache Hayati  Maalim Seif  Sharif  Hamad apumzike  peponi .

Aidha, CCM  kimetaja kwa mujibu  wa Katiba ya Zanzibar  ya Mwaka  1984, kupitia mabadiliko ya kumi ya katiba ya Zanzibar, hakuna chama cha siasa  kinachounda Serikali peke  yake bila kuvishirikisha vyama vingine  .

Akizungumza   katika Afisi kuu ya CCM  Kisiwandui ,Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo, Khamisi  Mbeto  Khamis ,amesema anachodai Othman  kuwa Serilali ya Zanzibar  ni CCM  peke yake anaonyesha   kuchanganyikiwa.

Mbeto alisema inasikitisha  kumsikia Kiongozi   aliyekuwa akiheshimika toka  akiwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Mashitaka baadae kuwa Mwanasheria Mkuuu SMZ  ,akiamua kuwa muongo  namba moja Zanzibar.

Alisema Serikali  ya Awamu ya Nane Zanzibar,  imeundwa na Vyama vitatu , CCM, ACT  Wazalendo na ADA Tadea  hivyo  kudai   miaka mitano iliopita  ilikuwa ni Serikali ya CCM peke  yake, huo  ni zaidi ya uongo.

"Othman kama  hana maneno ya kuwaeleza  Wazanzibari alipumzishe kulitaja  jina la Hayati Maalim  Seif kila  wakati .Aseme lipi jipya  atalofanya ambalo Dk Mwinyi bado  hajatekeleza  . Mwambieni asiwe  kama kasuku anayekariri maneno hayo kwa hayo   "Alisema  Mbeto  

Vile ville , Katibu Mwenezi  huyo alisema Othman  ndiye  Mshauri Namba moja wa Rais Dk Mwinyi  akiwa Makamo wake wa kwanza  wa Rais  hivyo  kama kweli ingekuwa hakubaliani na maamuzi ya SMZ , angepinga akiwa ndani ya kiiko cha Baraza la Mapinduzi .

"Mipango ,mikakati na maamuzi  yote ya SMZ  hupitishwa na kikao cha Baraza la Mapinduzi. OMO  ni Makamo wa Kwanza wa Rais. Angekuwa mpinzani wa sera na  mipango ya Serikali angekataa kuidhinisha ndani ya Baraza la mawaziri  "Alisisitiza 

Mbeto alisema kitendo cha Makamo huyo wa Kwanza wa Rais  kusimama  hadharani na kudai mipango yote  imefanywa na Serikali ya  CCM si kweli kwakuwa  ACT  ni mshirika wa SMZ,hivyo  kudai hakikushirikishwa ni usaliti mpya. 

"Mfikishieni salamu OMO ajiamini kusimama kwa kutumia miguu  yake na kujenga hoja. Ikiwa kila akisimama analitaja jina la Maalim Seiif anaithibitishia dunia ni  Kiongozi  dhaifu asiyejiweza kwa lolote " Alieleza Mbeto

No comments