DKT.NDUMARO ASIFIA UTENDAJI KAZI OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
Na Mussa Augustine.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro amesema kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo,Mwaka huu wa fedha 2025/2026 imetenga fedha kwa ajili ya kufanya ufasili wa Sheria zipatazo 146 ambazo zilikua bado hazijatafsiliwa kutoka lugha ya kingereza hadi kiswahili.
Dkt.Ndumbaro amesema hayo leo Julai 11,2025 wakati alipotembelea Banda la Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria(OCPD)katika Maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara(Sabasaba)yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere barabara ya Kilwa Kurasini Jijini Dar es salaam.
Aidha Dkt.Ndumbaro amesema kuwa Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria ina Mchangao mkubwa katika mchakato mzima wa utunzi na urekebu wa Sheria.
"Bila Ofisi hii(OCPD)hakuna Sheria inayoenda kutungwa bungeni,bila Ofisi hii hakuna Sheria ambayo inafanyiwa marekebisho,bila Ofisi hii hakuna Sheria ndogo inatungwa,bila ofisi hii hakuna Sheria ambayo itafanyiwa urekebu, kwahiyo ni Ofisi muhimu sana sana sana. "amesema
Nakuongeza"ikifa ofisi hii ina maana hata Mahakama itavurugikiwa,itakua inatumia sheria ambazo sio sahihi,ni Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria inayotuambia sheria sahihi,sheria hii niya Mwaka huu,nakwa toleo hili lenye urekebu wa Mwaka huu."
Amesema kuwa Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa sheria inafanya kazi nzuri ya kufasili Sheria kutoka kingereza hadi kiswahili,ambapo mpaka kufikia Juni 30 Mwaka huu wameshatafsiri sheria 300 kati ya Sheria 446,ambapo sheria 146 zitatafsiliwa katika Mwaka huu wa fedha 2024/2026 ili wananchi waweze kuzielewa.
"Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria ni Ofisi muhimu sana katika mstakabali mzima wa kutunga na kuchakata Sheria za Nchi,amesisitiza Dkt. Ndumbaro.
DKT.NDUMARO ASIFIA UTENDAJI KAZI OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
Reviewed by mashala
on
14:21:00
Rating: 5
Reviewed by mashala
on
14:21:00
Rating: 5



No comments
Post a Comment