MWANACHAMA JUMUIYA YA WANAWAKE KATA YA UKONGA MAGRETH SIDODO ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UDIWANI VITI MAALUMU
Na Mwandishi Wetu.
Mwanachama wa Jumuiya ya wanawake kata ya Ukonga Wilaya ya Ilala Magreth Gudiluck Sidodo amechukua fomu ya kugombea Udiwani wa Viti maalumu.
Magreth Sidodo amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Ilala Rosemary Mwakisalu Ofisini kwake Ilala Dar es salaam.
Magreth Sidodo amesema ameamua kuomba ridhaa ya kugombea nafasi hiyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

No comments
Post a Comment