Zinazobamba

MTAALAMU WA FEDHA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MASSOUD MAPANDE ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIVULE

Na Mwandishi wetu

Mtaalamu wa Masuala ya Uchumi na Fedha kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mosoud Mapande amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mapande amechukua fomu mapema leo Juni 29,2025 na kukabidhiwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Sylvester Yeredi 

Amesema endapo atapitishwa na chama Chake cha CCM atahakikisha  anamsaidia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo.

.

No comments