Zinazobamba

Mbeto : Watanzania kataeni kugawanywa kwa Udini na Ukabila


Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakuna na wala hatokei mtu  yeyote  atakayethubutu kuwagawa Watanzania  aidha kwa ushawishi wa Dini, Ukabila au Ukanda.

Chama  hicho pia kimewahakikishia Watanzania , Amani na Umoja  wa Kitaifa uliojengeka ,hakutokani na dhamana ya  mtu mmoja ,  dini fulani, kabila au kanda  yoyote. 

Katibu wa Kamati  Maalum ya NEC  Zanzibar , Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis ameeleza hayo  huku akiahidi hatokei yeyote mwenye  misuli ya  kulipasua Taifa. 

Mbeto  alisema kutokana na Waasisi wa taifa kutoa jasho  jingi  ,kupoteza ,maishha , nguvu na jasho lao  jingi ,hakuna Mtanzania  aliye  tayari kuona Taifa  likigawanywa na vibaraka wachache.

Alisema Tanzania  imejengwa kwa nguvu  ya Dini  zote, Makabila na Wananchi kuanzia Vijiji ,Kata,  Wilaya na Mikoa  yote,  hivyo dhamana ya kulihami na kulilinda Taifa hili ,  itabaki mikononi  mwao wenyewe. 

'Chama chetu  kinawahakikshia   hatatokea  mtu  yeyote  au kikundi  litakalowagawa Watanzania  aidha kwa ushabiki wa Dini, Ukabila au Ukanda. Taifa letu  litaendelea kubaki imara na kuwa  moja  milele' Alisema Mbeto 

Aidha, Katibu  huyo  Mwenezi  aliongeza kusema na kutaja hatua ya  kuchomoza kedi na   vitimbi vya  baadhi ya  watu  wanaodhani wana ubavu wa kukoleza kuni za  uchochezi huku akisema watu hao  wataaibika.

"Tumeshuhudia yaliotokea kwa majirani  zetu  pia  Taifa la Afrika ya Kati. Tunajua  hatari na hasara ya mivutano ya Udini na Ukabila . Hakuna atakayelala kitandani kwake akawaacha manyang'au wakilipasua Taifa "Alisisitiza Mbeto 

Aidha alisema  wakati huu  nchi ikielekea  katika Uchaguzi  mkuu, watachomoza  watu mapepe watakaofanya majaribu wakidhani dola itakuwa imelala , hivyo akawataka wajue kila  dola  duniani ina pua zake, macho, midomo  na masiko . 

"Tulumbane na kucharuana  kwenye majukwaa ya Kisiasa bila kuamsha hisia za dini, ukabila au ukanda. Atakaepita kwenye barabara hizo atakutana na baladia zenye miba na misumari " Alieleza 

Akizungumza kwa undani, Mbeto  alisema ikiwa kuna Wanasiasa ambao waliopeteza amana na mtaji ya kisiasa katika jamii, waache kutumia Lugha za ukabila na udini kwani hayupo atakayewavumilia.

Mbeto alisema Watanzania  ni werevu  hivyo hawako tayari kutumika katika ushabiki wa  hovyo huku  wakiliacha Taifa lao likipoteza Amani ,Umoja na Mshikamano.

No comments