Zinazobamba

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA KUANZA JUNI 16,2025 MKOANI DAR ES SALAAM.


Na Mussa Augustine.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka wananchi wenye changamoto za kisheria Mkoani humo kuhakikisha wanajitokeza kwenye kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia Suluhu Hassan itakayoanza Juni 16,2025,Mkoani humo. 

RC Chalamila ametoa rai hiyo leo Juni 13,2025 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na kampeni hiyo ambayo ina lengo la kutoa masuluhuisho ya kisheria kwa ajili ya kutoa haki kwa Wananchi. 

Aidha amesema kuwa Dar es salaam ni miongoni mwa Mikoa ambayo imekua ikiripotiwa kuwepo kwa ukatili wa kijinsia kwa watoto na watu wazima, pamoja na kuwepo kwa Migogoro mbalimbali ya kisheria. 

Aidha amesema kuwa maeneo ya Migogoro ya kisheria ni pamoja na Migogoro ya Ndoa,Ardhi,Mirathi,huku akiwasisitiza Wananchi kuhakikisha wanakuja na nyaraka zote muhimu kwa ajili ya kushughulikia madai yake na kupata haki anayostahili kwa mujibu wa Sheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Sheria na Katiba Ester Msambazi amesema kuwa tangu kuanza kwa kampeni hiyo Mwaka 2023 imefanikiwa kutafuta Migogoro 5000 ya moja kwa moja pamoja na kuwafiakia watu zaidi ya milioni 40 kupitia vyombo vya habari.


No comments