HANANJA AMRIPUA GWAJIMA,ASEMA KAULI ZAKE KUHUSU UTEKAJI NI UCHOCHEZI.

*Awataka Watanzania kuendelea kushikamana kulinda Tunu za Taifa ikiwemo Amani.
Na Mwandishi Wetu
Hananja ametoa matamshi hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari nakubainisha kwamba hatua hiyo inayoendelea sio sahihi,hivyo inapaswa masuala ya udini yaachwe ili kulinusuru Taifa lisingie kwenye Migogoro ya uvunjifu wa amani.
Aidha ameendelea kusema kuwa madhabahu ni sehemu ya kusememea na kukemea mambo maovu lakini inapaswa mambo hayo yasemwe kwa lugha ya staha na sio kwa njia ya uchonganishi.
"Nakubali kabisa kwamba Madhabahu ni sehemu ya kusemea mambo mbalimbali lakini unasemea kwa lugha gani?..ipi nafasi yako?.. hivyo chunga sana nafasi yako uliyonayo" amesema Hananja.
Nakuongeza kuwa "Mimi nayajua mabomu, nazijua bunduki toka muda mrefu, saivi tunakaribisha mafarakano, cheche hizi zinaleta mafarakano ambayo yatasabaisha kukosekana kwa amani,hata kuabudu tutashindwa kama amani haitakuwepo".
Akizungumzia kuhusu kufungwa kwa kanisa la Ufufuo na Uzima , Mchungaji Hananja amesema kuwa hatua zilizochukulia ni sahihi kwani kanisa hilo halijasajiliwa.
" Kufungwa kwa kanisa ni sahihi, kanisa halijasajiliwa,pale hajasajiliwa Gwajima bali limesajiliwa kanisa,natumaini hawa ambao wanakiuka Sheria wapigwe pini(wafungiwe)vikanisa vyao visivyoeleweka,ukisajiwa unapaswa kufuata utaratibu" amesema Mchungaji Hananja.
HANANJA AMRIPUA GWAJIMA,ASEMA KAULI ZAKE KUHUSU UTEKAJI NI UCHOCHEZI.
Reviewed by mashala
on
13:40:00
Rating: 5
Reviewed by mashala
on
13:40:00
Rating: 5
No comments
Post a Comment