Zinazobamba

D Voice kufanya shoo ya Muziki wa Singeli Kanda ya Ziwa.


Na Mussa Augustine.

Msanii wa Muziki wa Singeli Divoice kutoka lebo ya WCB anatarajia kufanya shoo ya kibabe Kanda ya Ziwa.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mapema leo Juni 4 ,2025 Mtangazaji wa Wasafi Media ambaye pia ni C.E.O wa 7Media Kreiton Revocatus "Baba levo" amesema kwamba shoo hiyo itakua ya aina yake hivyo wakazi wa Mikoa ya Shinyanga,Singida na Mwanza wasikose burudani hiyo.

"Leo nimekaa hapa kama balozi wa Mandasi Store kampuni inayokopesha simu,kisha Mtanzania analipa kidogo kidogo,shoo hii imedhaminiwa na Mandasi Store"amesema baba levo.
Nakuongeza kuwa" D voice ni moja ya wa saini wenye nguvu kwa jamii ya Kitanzania kwenye international level ni Devoice kutoka level ya WCB,hivyo ameamua kufanya shoo kanda ya Ziwa ili kupeleka Muziki wa singeli."

Aidha Baba levo amesema kuwa shoo hiyo imedhaminiwa na Mandasi Store kwa lengo la kumsapoti msanii huyo kutoka WCB,ili kumuunga mkono Diamond Platinums katika kuinua muziki hapa nchini.

"Mandasi Store tunakufa na D voice ambapo tarehe 6 tunaanza pale Shinyanga ukumbi wa Izi piano,watu wote wa Shinyanga tunawaletea Divorce make mako wa kula."amesema 

Nakuongeza kuwa " Tukitoka Shinyanga Juni 7 tutakua Manyoni( Singida)tukiwa hapo watu wa Manyoni watapata show kubwa tutahakikisha watu waanyoni wanakopeshwa simu wanalipa kidogokidogo."

Aidha ameongeza kuwa Juni 8 shoo hiyo itafanyika Mwanza,hivyo mashabiki wa Muziki wa singeli Mkoani huo wajitokeze kwa wingi ambapo pia watakopeshwa simu ili walipe kidogokidogo.



No comments