Zinazobamba

WAZIRI MKENDA AITAKA HESLB KUWEKA MIFUMO INAYOSOMANA NA MAMLAKA ZINGINE ZA ELIMU.


                  Profesa Adolf Mkenda

Na Mussa Augustine.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameielekeza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu( HESLB) kuhakikisha inaweka mifumo inayosomana na mamlaka zingine za Elimu ikiwemo Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA )na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET)ili kusaidia kutoa huduma bora kwa wateja.

Waziri Mkenda ametoa maelekezo hayo leo Maei 15,Jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano wa wadau mbalimbali wa Elimu,waliokutana katika Mkutano  ulioandaliwa na HESLB kwa kushirikiana na Adapt IT kwa lengo la kujadiliana kwa pamoja namna ya kuboresha mifumo ya kidijitali kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wanafunzi.

Profesa Mkenda amesema kwamba mifumo ya kidijitali imekua ikisaidia kutoa huduma kwa ubora nakwa wakati,hivyo HESLB haina budi kua na mifumo ambayo inasomana kwa pamoja na mamlaka zingine ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wateja.

"Napenda kutumia fursa hii kuwapongeza Bodi ya Mikopo kuandaa Mkutano huu na kukutanisha Wataalamu wa ndani na nje wenye uzoefu katika mifumo ya kidijitali,hivyo naamini maamuzi mtakayofikia katika majadiliano yenu yatawezesha kupata solutions mbalimbali za changamoto za mifumo ya kidijitali." amesisitiza Prof Mkenda.
                         Dkt.Bill Kiwia
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa HESLB Dkt.Bill Kiwia amesema kwamba Bod ya Mikopo ya Elimu ya juu itatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkenda ili kuweza kufikia malengo yaliyokusuduwa na Serikali katika utoaji wa huduma bora kwa wateja.

"Mkutano huu umewaleta wadau kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na Adapt IT ili kujadili hizi changamoto na namna ya kuja na njia nzuri ya kuweza kuboresha huduma zetu." Dkt.Kiwia

Nakufafanua," Lengo la kuwaleta hawa Adapt IT ,wameshafanya kazi kwa muda wa miaka 40 katika nchi mbalimbali, na wamekua wakishirikiana sio tu Afrika hata Ulaya, Australia, Singapore na nchi zingine, kwahiyo wenzetu hawa wanauzoefu tunakaa nao, tunajadiliana nao na baada ya hapo tunakuja na mapendekezo ya kuboresha kile tunachokifanya,au kama sio kuboresha basi kukiweka kitu kiwe bora zaidi ili tuweze kutoa huduma bora kwa wateja Wetu."
Aidha amesema kuwa mifumo hiyo inasaidia kumtambua  mwanafunzi tangu akiwa darasa la kwanza ili akifika  hatua ya chuo kikuu HESLB ambayo ndio inayonufaika na mfumo huo iweze kumchukua na kumpeleka kupata mikopo kwa wakati unaostahili nakwa huduma anayohitaji.

Aidha amesema kuwa hatui hiyo ni sehemu ya maoni ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,pamoja na  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye amekua akisisitiza kutengenezwa mifumo itakayo somana na vilevile teknolojia iwe ni  chachu ya maendeleo



No comments