Zinazobamba

MKE WA RAIS WA FINLAND ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA.


Na Mussa Augustine.

Tanzania na Finland zimekua na ushirikiano mzuri katika sekta mbalimbali ikiwemo ikiwemo Sekta ya Misitu pamoja na kubadilishana Wataalamu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 14,2025 Jijini Dar es salaam  na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Hassan Abbas baada ya mke wa rais wa Finland kutembelea Makumbusho ya Taifa ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo pamoja na utamaduni wa mali kale.

Aidha Dkt.Abbas amesema kuwa katika ziara hiyo fupi ya Rais wa Finland kutembelea nchi ya Tanzania itawezesha pia  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuzindua mradi wa kiasi cha Dola Paund milioni 20 ambapo ni  mradi mpya utakaosaidia kukuza na kuendeleza Sekta ya Misitu Nchini Tanzania.
"Nchi yetu imekua na mashirikiano makubwa na nchi ya Finland kwani sisi ni marafiki wa muda mrefu ambapo hata Rais Hayyat Mwl Julius Nyerere miongoni mwa ziara zake za mwaka 1973 alitembelea nchini Finland"amesema Dkt.Abbas.

Nakuongeza kuwa" Sisi wizara ya mali asili na utalii tunanufaika sana na wenzetu wa Finland hasa katika sekta ya Misitu,tuna ushirikiano wa zaidi ya miaka 40,miradi ambayo tumekuwa tukiifanya inayohusu misitu na mazao yake,huu mradi ambao tutausaini kesho kutwa ni muendelezo wa haya yote ambayo wamekuwa wakitusidia."
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema ujio wa mke wa rais wa Finland ni mafanikio makubwa ya Serikali ya awamu ya sita katika kuutangaza utalii lakini pia ni alama kwa Wizara ya Maliasili na Utalii katika kupanua wigo wa kutangaza vivutio vya utalii.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni hamasa kwa watanzania  na wageni waendelee kutembelea makumbusho ya taifa kwa ajili ya kujifunza historia ya taifa, utamaduni na urithi,pamoja na kufahamu muingiliano wa nchi hizo na Mataifa mengine na mashirikiano mazuri baina ya nchi na Mataifa mengine

"Makumbusho ya taifa tunashughulika  na tafiti,ukusanyaji,uendelezaji na kutoa elimu kwa Jamii kuhusu mambo mbalimbali ya kale,hivyo tunapeda kushirikiana na nchi ya Finland  katika kufanya utafifi katika eneo la tamaduni na mali kale kwani wao wamepiga hatua katika eneo hilo".amesema Dkt.Lwoga

Nakuongeza kuwa,"pia ujio wa Rais wa Finland kesho kutembelea makumbusho ya Taifa si tu kuacha alama ya  mashirikiano mazuri yaliopo baina ya nchi zetu  bali kuwakumbusha watanzania kupenda na kuthamini vitu vya kwao."


No comments