WAMACHINGA WAPEWE KIPAUMBELE JANGWANI:MCHENGERWA.
Waziri Mohamed Mchengerwa
Na Mussa Augustine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ametoa maelekezo kwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha wafanyabiashara wadogo(MACHINGA)wanapewa kipaumbele kwenye mradi wa mji wa kisisa Jangwani ambao unatarjiwa kuanza kujengwa hivi karibuni.
Waziri Mchengerwa ametoa maagizo hayo leo 24,2025 katika Kongamano la Wamachinga lilofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam nakubainisha ujenzi wa Mradi huo utazingatia kuwepo kwa maeneo ambayo yatatumiwa na Wamachinga kufanya shughuli za kibiashara kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
"Serikali haitarudi nyuma itakuwa bega kwa bega na wamachinga katika kuwabeba kuhakikisha wanatendewa haki na kuondoa unyonge vipindi vyote vya ukombozi dhidi ya kundi hili.
"Serikali ipo nanyi hivyo msikubali kutumiwa katika siasa nyepesi hadi mnafikia hatua ya kuandamana kwa maslahi yao, wakitaka kuandamana waacheni wao waandamane na familia zao".amesema Dkt Mchengerwa.
Aidha Waziri huyo wa TAMISEMI amesema kuwa makundi ya Wamachinga,Mama lishe pamoja bodaboda yaachwe yafanye biashara kwenye mazingira ya amani na salama katika kujiletea maendeleo,nakwamba hatua hiyo inasaidia kupunguza wimbi la vijana wasiokua na ajira mtaani.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema kuwa Machinga ni kundi maalumu ambalo linahitaji usaidizi wa Serikali ili mipango yao ya kibiashara iweze kusonga mbele.
RC Chalamila amesema kuwa idadi kubwa ya Wamachinga ni wabunifu katika kuinua biashara zao,pamoja na kufanya biashara wezeshi katika Mazingira rafiki na kuweka mikakati thabiti yenye lengo la kuinua uchumi wao.
Steven Lusinde
Naye Mwenyekiti wa Machinga Taifa Steven Lusinde amesema kuwa kundi la Wamachinga lipo tayari kulipa kodi kwa ajili ya kusaidia Serikali kuingiza mapato ya kuleta maendeleo ya Taifa.
WAMACHINGA WAPEWE KIPAUMBELE JANGWANI:MCHENGERWA.
Reviewed by mashala
on
18:00:00
Rating: 5

No comments
Post a Comment