Zinazobamba

WAKILI NDELWA: INEC IENDELEE KUTOA ELIMU KWA VYAMA VYA SIASA JUU YA KANUNI ZA UCHAGUZI MKUU.

Na Mussa Augustine.

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeshauriwa  kuendelea kutoa elimu kuhusu kanuni za uchaguzi  kwa vyama vya siasa  kuelekea uchaguzi mkuu unaofanyika Oktoba Mwaka huu. 

Ushauri huo umetolewa leo Mei 2,2025 na Wakili na Mshauri Wakili wa Mahakama Kuu Mh.Lwijiso Ndwela wakati wa mahojiano na Waandishi wa habari kando ya mjadala wa "Cafe Talk"ulioandaliwa na Clouds Media,kwa kushirikiana na Crowns Media pamoja Ayo Tv.

Aidha amesema kuwa Wakati huu wa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani vyama vya siasa vinapaswa kuwa na uelewa wa kina juu ya kanuni hizo hivyo INEC kwa kushirikiana na wadau wengine inapaswa kuendelea kutoa elimu ya kanuni za uchaguzi.
Wakili Ndelwa amesema kwamba pamoja na INEC kuweka wazi kanuni hizo baadhi ya viongozi wa  vyama vya siasa bado hawana uelewa mpana hivyo elimu inahitajika kuendelea kutolewa kwa Viongozi wa vyama hivyo.

"Napenda kuishauri Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi iendelee kutoa Elimu ili kuondoa sintofahamu kwa Viongozi wa vyama vya siasa juu ya kanuni za uchaguzi,na kuepukana na malalamiko ya hapa na pale pindi chama kinapoenda kinyume na kanuni hizo" amesema.

Nakuongeza kuwa" muda uliobaki ni mchache kuelekea kuanza kampeni na kufanyika uchaguzi,hivyo rai yangu kwa vyama vya siasa visome  kanuni hizi ili viepukane na kazia inayoweza kujitokeza wakati wa mchakato wa uchaguzi utakapoanza.
Mjadala wa " Cafe Talk"umefanyika katika hotel ya Serena Jijini Dar es salaam nakuhudhuriwa na Wadau mbalimbali ikiwemo Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

No comments