Zinazobamba

WAKILI NDELWA ASEMA KANUNI ZA UCHAGUZI ZIMEWEKWA WAZI.


*Asema chama kisiposaini kanuni hizo hakiwezi kushiriki uchaguzi mkuu.


*Avishauri vyama vya siasa kuzisoma vyema kanuni za maadili ya uchaguzi ili kuepuka kadhia ambazo wanaweza kukutana nazo.


Na Mussa Augustine.

Imeelezwa  kuwa kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani zimeweka wazi kuwa chama ambacho hakijasaini fomu za kanuni za maadili  hakiwezi kupata fursa ya kushiriki mchakato wa uchaguzi.

Hayo yamesemwa leo Mei 02,2025 na Wakili na Mshauri wakili wa Mahakama kuu Mh.Lwijiso Ndwela wakati  akihojiwa na waandishi wa  habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari  kwenye mjadala unaojulikana kama "Cafe Talk" ulioandaliwa na Clouds Media kwa kushirikiana na Crown Media na Ayo Tv ili kujadili juu ya kanuni za uchaguzi zinazosimamiwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi( INEC)

Wakili Ndelwa amesema kwamba kanuni hizo zinasema kuwa chama ambacho hakitasaini kanuni za uchaguzi hakitashiriki katika mchakato wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu,lakini haijasema hayo moja kwa moja.
"Ni muhimu kwa vyama vya siasa kuzisoma vyema kanuni za maadili ya uchaguzi ili kuepuka kadhia ambazo wanaweza kukutana nazo katika mchakato wa uchaguzi baada ya kushindwa kusaini kanuni hizo" amesema.

Mjadala huo wa cafe talk umeandaliwa na watangazaji nguli hapa nchini akiwemo Sudi Kipanya wa Clouds Media pamoja na Salimu Kikeke kutoka Crown Media umefanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wanasheria mbalimbali na Wadau mbalimbali wa habari. 


No comments