Zinazobamba

VIJANA WACHEKESHAJI WATAKIWA FURAHA FM.

Mkurugenzi Mtendaji Furaha Media,Bw.Furaha Dominic akizungumza na Waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusu fursa ya kutafuta Vijana wenye kipaji cha uchekeshaji(Comedians)

.Lengo ni kukuza vipaji vyao nakupata  ajira itakayowanufaisha maishani mwao.

Na Mussa Augustine.

Vijana wenye kipaji Cha uchekeshaji( Comedy)kutoka maeneo mbalimbali nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kinyanga'nyiro cha kutafuta nafasi ya ajira ya utangazaji wa kipindi cha uchekeshaji katika kituo cha Radio Furaha jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 27, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Furaha Media ,Bw.Furaha Dominic wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya kituo hicho yaliyopo Mikocheni  Wilayani Kinondoni Jijini Dar es salaam,nakubainisha kwamba lengo la kutafuta Vijana hao ni kuweza kuwasidia kuendeleza vipaji vyao pamoja na kuwapatia ajira.

"Mchakato wa maombi tayari umeshaanza,vijana wote wenye uwezo wa kuchekesha,kutoka nchi nzima wajitokeze kuomba nafasi hiyo ili kupata vijana wengi wenye uwezo wa kufanya kipindi cha vichekesho kupitia utangazaji wa radio"amesema Furaha kwa bashasha.

Nakuongeza kuwa"Lengo la kutoa nafasi hizi kwa watanzania hususani vijana ni kutengeneza ajira kwa kundi hili muhimu kwenye jamii,nimekua nikijitoa sana p kuwatafutia Vijana fursa mbalimbali ambazo zitawasaidia kupata ajira maeneo mbalimbali nakuweza kujikwamua kiuchumi kupitia vipaji vyao".

Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Furaha Media ikiwemo Furaha Fm na Furaha TV,ameongeza kwamba maombi ya nafasi ya uchekeshaji yanapatikana kupitia platform mbalimbali za kituo hicho, hivyo wachekeshaji  wanaotaka kutuma maombi yao wanatakiwa kuingia kwenye platform hizo  ili kufanikisha kutuma maombi yao.

Pia amebainisha kwamba kwa wale watakaofanikisha kutuma maombi hayo usaili(Interview)wa kuwapata wachekeshaji wa kipindi cha vichekesho (comedian presenter's)utafanyika rasmi Juni 11 na 12 Mwaka huu Jijini Dar es salaam huku akiwataka Vijana wenye vipaji kuchangamkia fursa hiyo mapema.

No comments