Zinazobamba

Mbeto :Uchaguzi ni mapambano ya ushindani wa sera na hoja si lelemama


Na Mwandishi  Wetu, Pemba

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Viongozi na wanachama wake kisiwani pemba kujiandaa  kisaikolojia na kujipanga kimkakati tayari  kushiriki  uchguzi  mkuu wa oktoba mwaka huu

Pia  chama   hicho kimesema  Uchaguzi  si jambo  dogo bali ni mapambano  ya  sera na hoja si kama kucheza  lelelmama au singeli.

Maelezo  hayo yametolewa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar  Idara  ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis  Mbeto  Khamis , alipozumgumza na  makundi ya viajna Wahamasishaji na Wasanii katika Ukumbi  wa Makonyo huko Wawi  Kisiwani hapa.

Mbeto alisema kila kiongozi  na Mwanachama kwa nafasi zao, wanatakiwa kuhahakikisha wanafanya kila linalowezekana  ili kupata ushindi wa kidemokrasia kwa kuwahamasisha wanachama na wananchi.

Alisema  matokeo  ya ushindi wa uchaguzi  ni  baada ya chama kutangaza sera zake ,wananchi kupiga kura ,kuhesabiwa na matokeo kutangazwa.

Alisema ni matarajio ya kila chama cha siasa kipate idadi kubwa ya kura  ,kwakuwa  wala Uchaguzi  si   simulizi za hadithi au maneno matupu.

'Chama chenu  kinawataka viongozi  wote  mjipange na kujiandaa kimkakati  kuelekea Oktoba Mwaka huu. Uchaguzi umeshapiga hodi hivyo lazima tukumbushane  mapema na kuanza  kujipanga "Alisema Mbeto. 

Aidha ,alisem pamoja na kila unapomalizika uchaguzi  mkuu mmoja , CCM  hujiandaa kwa uchaguzi mwingine, aliwataka wanachama kutobweteka na kufanya mambo kwa mazoea.

"Uchaguzi  hubadilika kulingana na mazingira husika.Hata  Malaria ukipima utakuta idadi ya juu au ya chini ya wadudu wake.Uzoefu katika kila uchaguzi  una  uzoefu na mazingira yake "Alisema  Mbeto 

Hivyo basi, Katibu  huyo Mwenezi  alisema hakuna  mtu mwenye  uwezo wa kufanya kazi peke yake bila kuwashirikisha wenzake  huku akiwataka viongozi wa CCM  kushirikiana na wanachama wao.

"Wasanii jiandaeni kutunga  mashairi ya nyimbo  nzuri za hamasa na kampeni .Wahamasishaji lazima mpite kila nyumba, kiambo kwa kiambo,shehia hadi shehia kuomba kura kwakuwa huo ni wajibu wa kidemokrasia  "Alieleza

Alisema  nyimbo zote zitakazotungwa zitahakikiwa  mapema na kupasishwa kabla ya kuimbwa , hivyo aliwataka watunzi wa nyimbo  hizo kuanza  kutunga mashairi  yatakayovutia na kuelimisha  wananchi kuhusu uchaguzi mkuu.

No comments