HESLB,NIDA KUANZA KUTUMIA NAMBA YA UTAMBULISHO UTOAJI MIKOPO YA ELIMU YA JUU.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt.Bill Kiwia( mwenye suti )kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA James Kaji wakizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matumizi ya namba ya utambulisho kwa ajili ya kuombea mikopo kwa wanafunzi.
Na Mussa Augustine.
Akizungumza mapema leo Mei 16,2025 Jijini Dar es salaam wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amesema kwamba kuanzia mwaka huu mpya wa masomo 2025/2026 namba ya Utambulisho itakua ni hitaji la lazima la kila muombaji mkopo atakae enda kuomba kupitia mifumo yetu ya Bodi hiyo.
Aidha Dkt.Kiwa amewashauri waombaji wote wa mikopo kuhakikisha wanapata namba za utambulisho mapema iwezekanavyo kabla ya dirisha la maombi halijafunguliwa na ndani ya muda wa maombi ya mkopo kabla ya dirisha la maombi halijafungwa.
"Hii namba ya Utambulisho( NIN)napenda kuutaarifu umma kwamba taasisi zetu hizi mbili(HESLB na NIDA)zimechukua hatua muhimu sana za kuhakikisha kazi hii inafanyika kwa ufanisi nakwa wakati,tayari tumeshaunganisha mifumo yetu inasomana "amesema Dkt. Kiwia.
Nakuongeza kuwa" Tumeamua kutumia namba ya Utambulisho( NIN) kwasababu ni namba ya utambulisho wa uhakika unaosaidia kupata uhalali wa taarifa za muombaji wa mkopo,pia itasaidia katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi yetu kutokana na kupata taarifa za uhakika naza kipekee za kila mwanafunzi

Amesema kwamba HESLB ina majukumu ya kutoa mikopo na kukusanya mikopo, hivyo kwa kutumia namba ya utambulisho(NIN) itaweza kuboresha uwezo wa kufuatilia nakuwapata wanufaika waliokopeshwa baada ya kuhitimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa( NIDA) James Kaji pamoja na mambo mengine amesema dhamira ya Serikali kwa ujumla ni kuona kila mwanafunzi aliyemaliza elimu ya Sekondari mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea na raia wa Tanzania,
anasajiliwa na kupata Namba ya Utambulisho( NIN) na kitambulisho cha Taifa itakayomwezesha kujiunga na masomo ya ngazi za juu na kati pamoja na kuomba mkopo wa masomo,pamoja na kupata huduma nyingine za kijamii na kiuchumi.
MD Kaji ameihakikishia Bodi ya Mikopo kuwa NIDA imejipanga kikamilifu kutoa huduma bora zaidi,na kuendelea kushirikiana kwa karibu na HESLB ili kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma za usajili kwa wakati ili waweze kufanikisha upatikanaji wa mikopo yao.
"Tunapofanya majukumu yetu yaliyo upande Wetu,niwaombe wanafunzi kwa upande wao nao watekeleze wajibu wao,kwa kuchukua hatua ya kujisajili mapema,msisubiri matukio kama hayo niliyoyataja ya kudahiliwa vyuoni au ajira ndipo mjitokeze ambapo muda unakuwa hautoshi lakini pia kuwafanya watumishi wa NIDA kuzidiwa kwa kuwa mnakuwa wengi kwa wakati mmoja" amesisitiza MD Kaji.
HESLB,NIDA KUANZA KUTUMIA NAMBA YA UTAMBULISHO UTOAJI MIKOPO YA ELIMU YA JUU.
Reviewed by mashala
on
16:04:00
Rating: 5

No comments
Post a Comment