Mbeto :OMO asiwanie urais zbar kwa kutegemea hadithi za vijiweni
Mweyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman , kutotia nia ya kuwania urais Zanzibar kwa kuziamini hadithi za kale za vijiweni na Mitaani zinazodai ati CCM hakijawahi kushinda.
Pia CCM kimekumbusha asidhani kwa kulitumia jina la Hayati Maalim Seif Sharif Hamad , kutamzidishia chochote ili akwepe kipigo cha kushindwa vibaya.
Hayo yameeelzwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis, aliyemtaka Othman, ajiandae kukumbwa na kimbunga kuliko kilichowahi kummkuta mgombea mwenzake wa upinzani
Mbeto alimtaka OMO aache kuziamini hadithi zinazodai CCM hakijawahi kushinda wakati ushindi wake ndio unaounda Serikali toka mwaka 1995 hadi sasa huku yeye (Othman) akiwa sehemu ya watumishi chini ya SMZ
Alisema ni upuuzi kwa mtu mzima kama Othman kuamini CCM hakitashinda wakati serikali ya CCM ndiyo inayomlipa mshahara ,imekuwa akimpatia nyumba anayoishi na familia yake , magari ,ulinzi na huduma nyingine muhimu .
'Othman jiandae kushindwa kama alivyushindwa mgombea mwenzako kuanzia mwaka 1995 hadi 2020. Kila CCM iliposhinda na kuunda Serikali wewe umekuwa kati ya watumishi wake watiifu SMZ waliopatiwa ajira " Alisema Mbeto
Pia Katibu huyo Mwenezi alisema madai ya kuwepo uvunjaji wa haki za binadamu na kutofanyika mageuzi ya kiuchumi ni maneno yasioingia akili wakati Zanzibar ya leo ikiizidi kumeremeta kimaendeleo .
'Acha kuwania urais wa Zanzibar kwa kutegemea ubebwe na jina la marehemu. Midhali umetaka uwekwe utangani na kufindwa, jiandae kuchezwa unyago waliochezwa wenzako "Alieleza
Mbeto alisema Othman ameamua kuchukua fomu ya kuwania urais katika wakati ambao smz chini ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi imefanya mageuzi makubwa ya kimifumo,kitaasisi ,kisheria na kuziweka sawa hali za maisha ya wananchi .
" Mgombea wa CCM hakumbushi tawala za kikoloni zilivyodumaza maendeleo ya Zanzibar .OMO anapokumbusha mambo yaliojiri mwaka 1995 nae akiwa sehemu ya smz ni kukichezea shere chama chake " Alisema
Katibu huyo Mwenezi alisema kama kweli Othman anaamini CCM ilikuwa ilisita nini kukubali teuzi alizopata ,akawa ana kula viapo na kuitumikia SMZ kwa utii na uaminifu.
'Hata kwa mtu anaedaiwa kueneza upekepeke wa CCM haijashinda uchaguzi aliajiriwa na SMZ ajira ya daraja la juu ,hakuwahi kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,si Mkurugenzi wala Mwenyekiti wa ZEC " Alisisitiza Mbeto
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni