Mbeto: CCM hakishabikii siasa za matabaka , ubaguzi na ukabila
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejipambanua si chama cha matabaka ya Ukanda, Udini na Ukabila ndio maana kilipinga Siasa za Ubaguzi wa rangi huko Afrika Kusini na kuwahifadhi Wapigania Uhuru .
Hivyo basi, kimewaasa watendaji wake ngazi za Matawi, Wadi,Majimbo, Wilaya na Mikoa , kufuata taratibu za kikatiba na kanuni ili kuendesha chaguzi zilizo Wazi, Huru na za Haki.
Indhari hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar ,Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis , alipozumgumza na wanachama pamoja na viongozi wa CCM.
Mbeto alisema ni mwiko na marufuku kwa Kiongozi au Mwanachama wa CCM , kutumia lugha ya ubaguzi ili achaguliwe, atakaebainika na kuthibitika amefanya hivyo ,matokeo ya ushindi wake yatafutwa .
Alisema kila mwanachama anatakiwa kufanya kampeni kwa kutumia mbinu halali za kidemokrasia hadi achaguliwe kwa ridhaa, akitumia ushawishi wake kisiasa , uwezo binafsi na upeo alionao.
'Hukuna atakaepata Uongozi kwa kutumia lugha ya ubaguzi aidha ya ubaguzi wa rangi, ukabila au kwa nasaba . Atakaefanya hivyo atakiuka misingi ya maadili na miiko ya chama .Matokeo ya ushindi wake hatutasita kuyafuta" Alisema Mbeto.
Aliongeza kusema CCM ni chama kilichoitangazia dunia kitapinga Siasa za Ubaguzi mahali popote duniani , kimefanya hivyo ikiwemo na kikivihifadhi vyama vya wapigania uhuru .
"Ardhi yetu imetumika na kuwa uwanja mapambano kwa vyama vilvyopigania uhuru vilivyopinga Siasa za kibaguzi . Tumefanya hivyo kwa kujiamini , dunia nzima inajua msimamo wa Tanzania chini ya sera za CCM "Alisistiza Mbeto.
Pia aliwakanya wanachama ambao hutegemea uwezo wao kiuchumi ili kurubuni watu wapiga kura wapate uongozi ,wasijisumbue kufanya hivyo kwakuwa hata wakishinda hawatapitishwa na vikao vya juu vya maamuzi.
Akisisitiza zaidi ,Mbeto alisema fedha kwa CCM si msingi wa maendeleo, ispokuwa heshima ya mtu mbele ya wenzake itokane na uzalendo wake, adabu na uaminifu wake .
"CCM ni chama cha Wakulima na Wafanyakazi. Uongozi si bidhaa au biashara mtu akidhani itanunuliwa. Wanachama wetu kataeni kuuza utu na heshima zenu kwa kutonunuliwa kama bidhaa sokoni " Alieleza.
Kadhalika ,Chama Cha Mapinduzi, hakitaona muhali wala aibu kukata majina yote ya wanachama watakaobanika kutumia rushwa kwa ajili ya kupata Udiwani, Uwakilishi na Ubunge
No comments
Post a Comment