Zinazobamba

MABATI ZONE YAVUTIWA NA MABADILIKO YA KIBIASHARA CHINI YA RAIS SAMIA, YAFUNGUKA KUHUSU USHIRIKIANO NA WATANZANIA

Na Mwandishi Wetu

Sekta ya ujenzi nchini Tanzania inaendelea kushamiri kwa kasi kubwa, huku wauzaji wa vifaa vya ujenzi wakizidi kuonyesha imani kwa serikali ya awamu ya sita. Mojawapo ya wadau wakubwa katika sekta hiyo ni kampuni ya Mabati Zone, inayojihusisha na uuzaji wa mabati ya viwango vya juu kwa bei rafiki kwa Watanzania.

Mikidadi Hassan Athumani, msambazaji mkuu wa mabati kupitia Mabati Zone na mfanyakazi wa kampuni ya Wachina ya Polaris, amesema serikali ya Rais Samia imefungua milango ya fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji kupitia maboresho ya sera za kodi na urahisishaji wa shughuli bandarini.

“Kwa sasa mizigo inatoka kwa wakati bandarini, jambo ambalo linapunguza gharama na usumbufu kwa wafanyabiashara kama sisi. Mazingira ya biashara yameboreshwa, na hii imeongeza imani kwa wawekezaji,” alieleza Mikidadi.

Kampuni hiyo, licha ya kuwa huru bila kuhusishwa na kampuni yoyote ya uzalishaji, inawakaribisha wawekezaji watakaopenda kushirikiana nao katika kuzalisha mabati hapa nchini, hususani Watanzania. Lengo lao kuu ni kukuza uchumi wa nchi kwa kushirikiana na wadau wa ndani.Kwa upande wake, Meneja wa Mabati Zone, Bi. Jacquline Swai, amesisitiza kuwa kampuni hiyo inatoa mabati ya kila aina, yenye ubora wa kimataifa, na huduma rafiki kwa wateja wake. Amesema wateja wanaonunua kutoka kwao hupata ofay a misumari bila malipo, usafirishaji wa bidhaa, pamoja na huduma ya kupata fundi wa kuezeka.

“Tunajali ubora wa bidhaa zetu na pia tunawajali wateja wetu. Hata zaidi, tunarudisha kwa jamii kwa njia ya misaada mbalimbali, kutembelea wagonjwa, yatima na wasiojiweza. Huu ndio moyo wa Mabati Zone,” alisema Jacquline.Kwa mahitaji ya mabati, wateja wanaweza kuwasiliana kupitia:0766 616 676

0665 508 173 au kutembelea ofisi za Mabati Zone zilizopo Tabata Matumbi, Dar es Salaam,

#fursa

#mabatiyatanzania

#raisamiahassan

#hudumabora

#mabatzone

#uchumimbadala

#watanzaniawazalendo

#viwandavyaNdani

#tanzaniainajengwa

No comments