Zinazobamba

Mbeto :Kauli ya Othman ni tangazo la fujo Zanzibar


Na  Mwandishi  Maalum ,Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema matamshi  yaliotamkwa na  Mwenyekiti  wa ACT  Wazalendo,Othman Masoud Othman, akidai muda wa maridhiano  umepita , sasa ni wakati  wa mapambano ni tangazo la fujo kabla ya oktoba mwaka huu.

Aidha  CCM  kimeyaita matamshi  hayo  yanachochea vurugu, ukorofi na ubabaiifu kuelekea  uchaguzi  mkuu oktoba mwaka huu baada ya ACT kubaini  hakina nafasi ya kushinda.

Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar  , Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamisi  Mbeto Khamis, aliyesema maridhiano ya kisiasa  na serikali ya Umoja  wa kitaifa  Zanzibar  yamefikiwa kwa mujibu  wa katiba na sheria.

Mbeto alisema  Zanzibar  kwa takriban  miaka mitano chini ya utawala wa Rais  Dk  Hussein Ali  Mwinyi, wananchi  wamekuwa wakiishi  kwa amani,umoja na maelewano tofauti na kabla ya wakati  wa  maridhiano  kufikiwa .

Alisema maelewano yaliopo Zanzibar ni baada ya kufikiwa na miafaka kadhaa ,hatimaye ndipo maridhiano   yalioridhiwa  na vyama vya CCM na CUF mwaka 2009 yakaunda SUK. .

"Bila shaka Othman  hatambui maridhiano  ya CUF kwakuwa ACT sicho   kilichofikia muafaka  .Hata hivyo  msimamo huo ni aina ya chochezi mpya  .Ikiwa  ACT kuna fukuto na mvutano asihamishie matatizo hayo kwa  wananchi " Alisema Mbeto. 

Katibu huyo Mwenezi  alisema  wananchi toka mwaka 2010 ,wamekuwa wakiishi  kwa maelewano imara hivyo hawako tayari  kugawanywa kwa namna  yoyote na kuirudisha  nyuma Zanzibar kimaendeleo  . 

Pia  Mbeto   alisema hata matamshi  ya Othman kumtaja  mkuu wa nchi  mwanamke  na kumwita  mwizi ,hayampi heshima Mwenyekiti  huyo wala chama chake  mbele ya jamii inayomtazama.

"Kumtaja kiongozi  mwenzako   kwa jinsia  yake ya kike au kiume ni kebehi na  dharau . Othman kama  atakuwa ndiye mgombea  urais wa ACT  ameshimdwa kabla ya  oktoba mwaka huu " Alieleza

Mbeto alisema   hatua ya ACT Wazalendo kudai  kitaongoza mapambano na kuweka kando  maridhiano, hakionyeshi nia njema na ukomavu  wa kisiasa  badala yake chama hicho kimejipanga kwa fujo.

" ACT Kutangaza hakitaki siasa za  maridhiano badala yale kitaendesha siasa za  mapambano ni ukiukaji wa matakwa ya  misingi ya demokrasia. Matamshi ya ACT yanavunja azma ya kulinda umoja na amani " Alisema

Mbeto  alisema hata kukitaja kikoa cga kamati kuuu ya ACT  kwamba kitatoa maelezo kuhusiana na hatua zaidi  zitakazochukuliwa  kuelekea oktoba ni jambo linalitia wasiwasi na hofu

Hakuna maoni