VIONGOZI WA DINI WAIOMBA SERIKALI KUUFUTA MTANDAO WA KIJAMII WA "X " (TWITTER) KUTOKANA NA KUHAMASISHA MAPENZI YA JINSIA MOJA.
Viongozi wa Dini nchini wamezitaka Mamlaka za serikali kuufungia
mtandao wa Kijamii wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter Kwa kuhamasisha
vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga)
Ombi hilo limetolewa leo Juni 11, 2024 Jijini Dar Es Salaam na Alhaj
Dkt Abdul Suleiman wakati akizungumza na waandishi wa habari nakubainisha
kwamba vitendo vya Mapenzi ya Jinsia
Moja (Ushoga ) vimepigwa marufuku hata
katika maandiko ya dini ya kiislam na kikristo ,hivyo vitendo hivyo
havikubaliki na vinapaswa kulaaniwa mara moja.
Dkt Sule amesema kwamba kufuatia Mtandao wa X ambao hapo zamani
ulijulikana kama “Twitter”kuruhusu kuchapisha maudhui yanayohamasisha vitendo
vya mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ushoga na usagaji Mamlaka zinazohusiana na
mawasiliano zinatakiwa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ikiwemo kufuta mtandao huo hapa nchini.
Kwa upande wake Askofu na Katibu mkuu wa Kanisa la Methodox
Tanzania Allen Siso amesema katika vitabu vya dini vyote havikubaliani na ndoa
za jinsia moja akitolea mfano kitabu cha Warumi 1:26 kinachosema 'hivyo Mungu
aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu,hata wanawake wakabadili matumizi ya asili
kwa matumizi yasiyo ya asili,na wanaume nao vivyo hivyo'.
Naye Sheikh Hilal Kipozeo amesema mtandao wa X unatakiwa kufutwa haraka iwezekanavyo,nakwamba ni vyema
kuundwa Sheria kali ya Kudhibiti mapenzi
ya jinsia moja na usagaji ili kusaidia kizazi kijacho kisiharibike.
“Mungu aliruhusu wanadamu wazaliane na wakaongezeke lakini hili
tatizo hata siku moja haliwezi kuruhusu wanadamu wakazaliana na kuongezeka
hivyo Mara moja mtandao wa X Ufungiwe"amesema
Naye mwakilishi wa walimu ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi
Gongolamboto,Munira Njau amesema kuwa wazazi wamekuwa na tabia za kuwaachia
watoto wao wachezee simu zao Hali iliyopelekea watoto kuingia kwenye mitandao
hiyo na Kujifunza tabia mbaya siku Hadi siku na hatimaye kuzipeleka mashuleni.
"sisi walimu tunashinda na watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni,na tunakutana na wanafunzi ambao tayari Wana viashiria vya tatizo hilo na tunapowahoji wanasema wamekuwa wakisema vimeanzia majumbani na wengine kupitia simu za wazazi wao,hivyo suala hili tuungane wote kusaidia watoto
No comments
Post a Comment