Zinazobamba

UVCCM WAITAKA SERIKALI KUUFUNGA MTANDAO WA X KUTOKANA NA MAUDHUI YAKE KUWA TOFAUTI NA MAADILI

                 Mwenyekiti wa UVCCM, Mohamed Kawaida 

Na Mussa Augustine

Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeiomba Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuufungia mtandao wa Twitter (X) kutokana na maudhui yake kutokuendana na mila na desturi za kitanzania .

Ombi hilo limetolewa leo Juni 11, 2024 Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa UVCCM, Mohamed Kawaida wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema dhamira ya maudhui ya mtandao wa Twitter maarufu X kwa sasa ni mbaya kutokana na kutokwendana na tamaduni za kitanzania.

“UVCCM imekuwa na utamaduni na kazi ya kuendelea kufuatilia malezi ya vijana wa kitanzania wote ikiwemo wa chama na wale waliopo nje ya chama,ambapo hivi karibuni UVCCM imepokea taarifa ya kushtusha kwamba  mtandao wa X umeruhusu kuchapisha maudhui ya kingono yasiyofaa kwenye mila na tamaduni zetu,” amesema.

Kawaida amesema kupitia Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikifungia mitandao yote yenye maudhui ya namna hiyo hivyo anaimani pia itaufungia mtandao huo.

“Sasa wakati umefika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuufungia mtandao huo kutokana na maudhui yake kutokwendana na mila na desturi zetu “amesema.

Aidha Kawaida amesisitiza kuwa lengo la kufugia mtandao huo (X) ni kulinda maadili ya vijana wa kitanzania na Tanzania kiujumla,kwani vijana ni taifa la kesho na ni viongozi wanaotarajiwa.

“Mitandao ya kijamii isiwe bora kuliko utanzania wetu na mila na desturi
najua kuna watu wataweka zogo …na vurugu hii isiturejeshe nyuma kufanya maamuzi ya Mila na desturi zetu”amesema.

Ameongeza kuwa zaidi ya watu laki tatu wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii huku asilimia kubwa ikiwa ni vijana.

“Mtandao huu umelenga kutuharibia Mila na desturi zetu kama watanzania sasa mtandao huu kwa nchi yetu umefika mwisho kutumika,” amesisitiza  Kawaida kwenye mkutano na wanahabri.

Nakuongeza kuwa "Vijana wote wa Tanzania wawe mstari wa mbele kukemea suala hilo ambalo limelenga kuvuruga tamaduni za kiafrika nchini kwetu,nakwamba endapo mitandao mingine itaibuka kufanya kama mtandao wa x nayo itachkuliwa hatua.

 

No comments