TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO YATOA BASKELI 250 KWA WATOTO WENYE UHITAJI
Na Mussa Augustine
Taasisi ya Ongea na Mwanao imetoa Baskeli zaWalemavu 250 ili kutomuacha Nyuma Mtoto Mwenye Wenye Ulemavu katika Kupata Elimu Nchini.
Akizungumza na Waandishi Wahabari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa taasisi hiyo Steve Nyerere amesema kuwa kume kuwa na Baadhi ya wazazi wakiume huwatelekeza Wake zao kwasababu ya kujifungua Mtoto Mwenye Uhitaji.
"Kuna Wanaume ni Wazembe katika kulea Watoto wenye Ulemavu hufikia kuwa kana kuwa mtoto mwenye Ulemavu si wake, lakini mtoto akiwa na hana ulemavu anamdai mwanamke kuwa mtoto ni wake"Alisema Mwenyekiti wa Taasisi Ongea na Mwanao Steve Nyerere.
Nyerere Aliongeza kuwa Hali ya Mtoto Mwenye Uhitaji haimzuii mtoto huyo kupata Elimu.
Alibainisha kuwa Kupata Mtoto Uhitaji ni Mipango ya Mungu nasio Mikosi na kuitaka jamii kuondoka na Dhana hiyo.
"Sisi tunahitaji kupeleka Mahitaji kwa Wenye uhitaji popote walipo hivyo tunaomba taasisi nyingine zituunge mkono"Asisitiza Steve Nyerere.
Katibu wa taasisi Ongea Na mwanao Evon Sherry amesema taasisi hiyo imetembelea mikoa mitano na kubakisha mikoa miwili kwa jili ya Viti mwendo kwa wahitaji.
Alisema kampeni ya "Baskeli yaShule ya Mama" inalenga kumsaidia mtoto mwenye uhitaji kupata Elimu.
"RaisDk.Samia Suluhu Hassan anawasaidia wakina mama katika sekta ya Afya,Maji lakini Sisi tumeamua kumtua mama mtoto mgongoni" Alisema Evon Sherry.
No comments
Post a Comment