Na Mussa Augustine.
Serikali imeshauriwa
kupeleka ndege ya mizigo Mkoani Mwanza ili kurahisisha usafirishaji wa Minofu
ya Samaki katika nchi za ulaya.
Ushauri huo imetolewa
Machi 26 ,2024 jijini Dar es salaam na Rais wa Chemba ya Biashara ,Viwanda na Kilimo Tanzania (
TCCIA) Vicent Minja wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya
kutoa tathmini ya ziara iliyofanywa na viongozi wa Chemba hiyo katika Mikoa
mbalimbali nakubaini Kuwepo kwa changamoto ya wafanyabiashara wa Minofu ya
Samaki kusafirisha kitoe hicho kutoka Mwanza kwenda Nchi za Ulaya.
Minja amesema kwamba
Wafanyabiashara hao wamekuwa wakienda kutumia Usafiri wa ndege katika nchi za
jirani ikiwemo Kenya kutokana na na kukosekana kwa ndege ya Mizigo Mkoani
Mwanza hivyo ameishauri Wizara ya Uchukuzi kupitia Shirika la Ndege Nchini ATCL
kupeleka ndege hiyo ili kurahisisha usafirishaji wa Minofu ya Samaki Nchi za
Ulaya.
Aidha Rais huyo wa
TCCIA ameiomba Serikali kupitia Halmashauri zake kuweka Mazingira Mazuri ya
usafi katika maeneo ya kuchakata Minofu ya Samaki kwani inahatarisha afya ya
Walaji wa Kitoeo hicho.
“Mikoa ya Kanda ya
Ziwa ikiwemo Kagera na Mwanza Viwanda vya kuchakata Minofu ya Samaki
vinachakata kwa kiwango kidogo sana kwani kuna uhaba wa samaki kuokana na
wavuvi kuenda kuuza samakai hao nchi za jirani”Amesema.
Nakuongeza kuwa “Wafanyabiashara
wa Minofu ya Samaki wanapata shida yakusafirisha minofu hiyo nchi za Ulaya
kwani hakuna ndege ya Mizigo kutoka Mwanza ,tunaishauri serikali kupitia
shirika la Ndege(ATCL)kupeleka ndege ya mizigo ili kurahisisha usafirishaji wa
minofu hiyo.
Katika hatua nyingine
Minja ameishauri Wizara ya Kilimo kukutana na wakulima wa korosho Mkoani Mtwara
ili kujadili Changamoto za mfumo wa stakabadhi gharani pamoja na uuzaji wa
mazao yao kwa njia masoko kupitia vyama vya ushirika AMCOS kwani mfumo huo
unalalamikiwa na wakulima wa korosho Mkoani Mtwara pamoja na wakulima wa
Choroko na Dengu Mkoani Shinyanga.Kwa mujibu wa Rais wa
TCCIA Bwana Minja amesema kuwa ziara hiyo imeanza februari 20 , 2024 na
inatarajia kukamilika Mei 6 ,2024 katika Mikoa yote nchini,nakwamba kwa Sasa
viongozi hao wametembelea Mikoa ya Dar es salaam,Pwani,Lindi,Mtwara,Shinyanga,Geita,Kagera,Mwanza,Simiyu,pamoja
na Mara ambapo wamebaini kuwa wafanyabishara wengi wanakumbwa na changamoto
mbalimbali.
"Kuwe na
utaratibu mzuri wa Masoko na Stakabadhi gharani ili kuleta manufaa kwa
wakulima ,hivyo Serikali ikutane na wakulima izungumze nao kujua changamoto
zinazowakabili”Amesema Minja.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni