Wanafunzi UDSM Wakoshwa na mradi wa LNG, Wapata elimu kuhusu PURA
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Kitivo cha Sayansi
ya Kilimo na Teknolojia ya vyakula wameelezea kufurahishwa kwao baada ya kufika
banda la PURA, huku wakisisitiza kuwa mradi wa LNG utasaidia kuinua uchumi wa
Watnzania.
Wanafunzi hao ambao wanasoma kozi ya Uchumi wa Kilimo,
Maliasili na Biashara wametembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu
wa Petroli (PURA) kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.
Katika banda hilo la PURA wamepata kujionea
fursa mbalimbali zinazopatikana katika taasisi hiyo ikiwemo kujifunza kwa
uhalisia.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao, Katibu
wa Chama chao (Dar es Salaam University Agribusiness and Natural Resources Economic
Association), Bw. Omary Mrisho alisema lengo la kutembelea banda hilo ni
kujifunza uhalisia wa kile ambacho wamekuwa wakikisoma darasani katika maisha
ya kawaida.
Alisema ziara hiyo wameweza kupata elimu kwa
uhalisia na kugundua ndani ya PURA kuna fursa nyingi za ajira kutokana na mfumo
wa mamlaka hiyo ya serikali.
Alisema,PURA ni miongoni mwa taasisi za
Serikali ambayo ina fursa nyingi za kutoa ajira nyingi kutokana na kiwango cha
elimu ya mtu, ikiwa ni pamoja na wenye ujuzi wa aina mbalimbali.
fursa nyingi na kazi ambazo imekuwa ikizifanya
ya utafutaji, uendelezaji kudhibiti na kubwa kinachohitajika ni mwamko mkubwa
wa watu kuja katika maonesho haya katika banda la PURA kuja kujifunza kwani
fursa zipo PURA,”amesema.
Aidha, aliwasihi wanafunzi wengine kuwa na
moyo wa kutaka kujifunza kitu badala ya kukaa darasani na kusubiri pekee watoke
nje ili wapate fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo na uhalisia wenyewe.
Naye Mkuu wa kitengo cha ushirikishwaji wazawa
na uhusishaji wadau kutoka PURA, Charles Nyangi amesema Mamlaka hiyo imepata
faraja na kunufaika katika maonesho hayo kwani watu mbalimbali wamepatiwa elimu
juu ya majukumu yake sambamba na kuwashirikisha fursa zinazopatikana PURA.


No comments
Post a Comment