Makamba aipongeza Tanesco katika maonyesho ya sabasaba
Mwandishi wetu
Waziri
wa Nishati January Makamba ameelezea kufarijika kwake baada ya watendaji wa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO,) wakijitoa kwa hali na mali kuwahudumia
wananchi.
Pia alisema
Shirika limejipanga kuwasiliana na kuwafikia wananchi sambamba na kupokeo kero,
changamoto na maoni ya wananchi na kuyapatia uvumbuzi.
Makamba Amebainisha
hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda la TANESCO
katika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba.
Makamba
alisema kuwa, Wizara na taasisi wameshiriki maonesho hayo ili kutoa elimu kwa
Umma wa Tanzania kuhusiana na majukumu yanayofanywa na Wizara pamoja na Taasisi
wanazozisimamia
”Tukiwa
kama Wizara, Serikali na taasisi ni jukumu letu kuhakikisha mawasiliano kwa
Umma ni muhimu ili wananchi waweze kuelewa ni nini tunafanya na hatua
zinazochukuliwa na wizara katika kuboresha huduma zinazotolewa na wizara pamoja
na taasisi zake.” Amesema.
Makamba alisema
amefarijika baada ya taasisi hizo na viongozi wake kushiriki kwa ukaribu zaidi
na kuwahudumia wananchi katika maonesho hayo kwa ukamilifu akiwemo Mkuregenzi
mkuu wa TANESCO Maharage Chande.
”Tunaona namna
suala hili lilivyo muhimu kwa Wizara na taasisi zote, mawasiliano, elimu na
huduma kwa Umma ni muhimu kwetu tunamwona MD Chande yupo hapa akishiriki kutoa
huduma kwa wananchi hii ni namna ambayo tumejipanga katika kuhakikisha kila
mwananchi anapata na kufikiwa na huduma kwa kiwango bora zaidi.” Ameeleza.
Waziri Makamba
ameeleza kuwa TANESCO ni shirika linalobadilika na limejipanga katika kuboresha
huduma na kurahisisha upatikanaji wa umeme na kusambaza umeme kwa gharama nafuu
nchi nzima.
”Ninafarijika na
mwenendo wa shirika, limekuwa zaidi ya shirika la kiufundi na uhandisi na
limekuwa shirika la kihuduma..Mwelekeo wa kihuduma unaonekana, mambo mazuri
yanakuja ndani ya miaka miwili, mitatu ijayo litakuwa shirika bora na lenye
viwango bora la utoaji huduma na mwelekeo wetu unakwenda sambamba na bajeti ya
wizara tuliyoitoa Bungeni kwa maslahi ya watanzania wote.” Amesema Makamba.
Akifafanua juu ya
kauli mbiu ya maonesho hayo ya ‘Tanzania ni Sehemu Sahihi kwa Biashara na
Uwekezaji’ Makamba amesema, huduma wezeshi za uwekezaji ni pamoja na nishati ya
umeme ya uhakika wakiwa kama sekta na watoa huduma hiyo (TANESCO,) wanafahamu
wajibu wa kujenga mazingira ya kuvutia wawekezaji kwa kuunga mkono jitihada za
Rais Samia Suhulu Hassani za kuitangaza nchi ulimwenguni.
”Tunaunga mkono
jitihahada zinazofanywa na Rais, sisi tunaosimamia sekta zinazovutia uwekezaji
tupo tayari, TANESCO wana miradi mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa umeme
ukiwemo mradi wa kimkakati wa Julius Nyerere na miradi mingine ya kuhakikisha
upatikanaji na usambazaji wa umeme ni wa uhakika… kazi tunazofanya zinasadifu
kauli mbiu ya maonesho haya.” Amesema.
Kwa upande wake
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO,) Maharage Chande amesema
wamejipanga kuwa shindani katika bara za Afrika kwa kuzalisha umeme kwa kiwango
cha juu na toshelevu kwa gharama himilivu za uzalishaji.
”Tuna miradi mingi
ya kuhakikisha nishati ya umeme inakuwa ya uhakika ikiwemo mradi wa kimkakati wa
Julius Nyerere utakaotumia maji na mingine itakayotumia gesi, tunaamini kupitia
miradi hii tutakuwa na umeme wa kutosha, bei himilivu na tutakuwa washindani
katika ukanda wa Afrika.” Amesema.
Chande amesema
shirika hilo lenye mitambo ya umeme yenye uwezo wa kuzalisha megawati 1700 ina
miradi ya umeme ya kuunganisha Tanzania na nchi nyingine katika Ukanda wa
Afrika ikiwemo Kenya, Zambia na Msumbiji na uwepo wa gesi ya kutosha nchini
utasaidia kuzalisha umeme mkubwa na kuweza kufanya biashara ya umeme kwa kushirikiana
na nchi za ukanda.
”Tunahitaji muda na
tunaamini tutafanikiwa kwa kiwango kikubwa na kuweza kuuza umeme katika nchi
jirani, muda mfupi wa kuzalisha umeme ni miezi 24 tena ni umeme wa nishati
jadidifu ya jua au upepo, na uzalishaji wa umeme wa maji huchukua takribani
miezi 36, 42 hadi 60 tuna mipango na juhudi katika kuhakikisha tunafanikisha
miradi ya namna hiyo kwa wakati ili tuwe shindani katika Kanda, taifa
lifanikiwe kwa kuwa na nishati ya uhakika na kwa gharama nafuu na kujenga
uchumi imara.” Amesema.

No comments
Post a Comment