Zinazobamba

Mamia ya wananchi wafurika Banda la PURA sabasaba

 



Na Mwandishai wetu

Viongozi mbalimbali kutoka Taasisi tofauti katika sekta ya mafuta na gesi wameungana na mamia ya washiriki wa maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba) kuhudhuria banda la PURA kujifunza na kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo.

Baadhi ya viongozi wa ngazi za juu waliotembelea banda hilo na kujifunza  ni pamoja na Mkugrugenzi Mtendaji wa Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC) Dr. James Mataragio Pamoja na Makamu  wa Rais wa Shell Exploration & Production Tanzania Ltd Bw. Jared Kuehl.

Viongozi hao warikaribisha na Mkurugenzi Mkuu wa PURA Injinia. Charles Sangweni ambaye alieleza kuwa dhumuni la kushiriki kwenye maonesho hayo ni kutoa elimu kwa umma kuhusu suala la Mafuta na gesi pamoja na fursa zinazopatikana kwenye sekta hiyo.

"Tumeshiriki kwenye maonesho haya kwa sababu ya kutoa elimu kwa watanzania kuhusu PURA, Kazi zake, fursa zilizopo katika sekta na jinsi ya kuzitumia ili kujiletea maendeleo,” alisema

Injinia. Sangweni alitumia fursa hiyo kueleza kuhusu mradi wa LNG, hasa fursa zilizopo mara tu utakapoanza kufanya kazi.

Alisema Ujenzi wa LNG unatarajia kuanza rasmi mwaka 2025, na katika kipindi hicho mradi unatarajiwa kutengeneza ajira 10,000 pamoja na ajira za moja kwa moja 600

"Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi pia kutakuwa na fursa mbalimbali ikiwamo ya kuuza huduma na bidhaa, mradi unafaida kubwa kwa umma,” aliongeza

Thamani ya mradi wa LNG unaelezwa kufikia Dola 30 Bilion sawa na Shilingi za Kitanzania Trilioni 72, unatarajiwa kuzalisha gasi kwa kipindi cha miaka 30

 

No comments