PURA wakaribisha wananchi sabasaba, Mradi LNG kuajiri watu 10,000
Na
Mwandishi wetu
Mwenyekiti
wa bodi ya PURA, Halfan Halfani amesema kuwa mradi wa LNG utasaidia kuongeza
ajira kwa watanzania ambapo watu takribani elfu kumi wanatarajiwa kupata ajira
hizo.
Alisema,kwenye mradi huo wafanyakazi wasiopungua 500, watapata kazi na
kwamba katika eneo hilo la mradi kutakuwa na ajira nyingi kwa watu wa bodaboda,
mama lishe pamoja na wajasiriamali wengine wa aina mbalimbali
Tanzania
inajipanga kuvuna neema ya gesi asilia katika mradi wa kuchakata na kusindika
gesi asilia(LNG), mradi ambao kampuni za wazawa zimepewa fursa ya kunufaika na mradi huo.
Wakizungumza
na vyombo vya habari katika maonyesho ya 46 ya biashara ya kimataifa Dar es
Salaam (DITF), kwenye banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu
wa Petroli (PURA), baadhi ya Makampuni ya wazawa walisema kuwa wameona thabiti
ya serikali katika kuhakikisha wazawa wananufaika kwenye fursa mbalimbali
zinazojitokeza katika sekta hiyo ikiwamo mradi wa mkubwa wa LNG.
“Mradi huu wa LNG utakuwa na tija kwa taifa kwani utadumu kwa zaidi ya miaka 50
huku tukitarajia kupata manufaa mara mbili, kwanza hela tutakayopata kwa kuuza
gesi ambayo itakuwa ikiuzwa mpaka nje ya nchi na kupata fedha za kigeni na pia
kwa kufanikisha nishati kwa viwanda, nyumba, magari na Taasisi za hapa
nyumbani na hivyo kutusaidia kufanya uzalishaji wa ndani” amesema Halfani.
Frank Mwankesi ni Mfanyakazi wa chama cha wafanyakazi cha mafuta na gesi
(OGAOGA) ameipongeza serikali kwa kuweka mazingira wezesha ya ajira
katika sekta ya madini na gesi.
Tumaini Abdallah ni mmoja wa vijana wanaofanyakazi kwenye
Kampuni za kizalendo zitakazonufaika na mradi wa LNG, ametoa shukrani kwa Pura
kwa kuziamini kampuni za ndani za uchimbaji wa gesi na mafuta na hivyo
kuaminika kwa Kampuni za kigeni zinazokuja kutekeleza uchimbaji wa gesi
asilia mkoani Lindi.
Tumaini
ametoa wito kwa Vijana wa Kitanzania kujitokeza kwa wingi kwenye fursa hiyo kwa
kuwa serikali ipo tayari kuwapa nafasi.
“Vijana
msiogope msaada upo na serikai ipo kwa ajiri yetu kama ambavyo sisi tumenufaika
kwenye mradi huu,"anasema Tumaini
ENDS,



.jpeg)
No comments
Post a Comment