FCC yawakaribisha wananchi sabasaba kupata elimu
| Mkurugenzi Uendeshaji wa Tume ya Ushindani (FCC ) Godfrey Machimu akiwajibika katika banda la FCC sabasaba, Machumu alisema Tume hiyo imejipanga kutoa elimu kuhusu shughuli mbalimbali wanazozifanya. |
| Afisa Uchunguzi wa FCC Waambie Malata akiwa katika banda tayari kwa majukumu yake, FCC imeweka banda lao katika ukumbi wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. |
| Afisa Kumlinda Mlaji katika Tume ya Ushindani Amina Mjungu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya tume hiyo. |
Na Mwandishi wetu
TUME ya Ushindani (FCC) imewshauri wananchi kupeleka
malalamiko yao yanayohusiana na changamoto za kibishara ili waweze kupata haki
yao ya msingi.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa uendeshaji wa Tume ya ushindani,
Godrfrey Machimu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya
46 ya Biashara ya Kimataifa, yanayoendelea viwanja vya Mwl. Nyerere Dar es
Salaam.
Tume ya ushindani imepiga kambi sabasaba ikiendelea kutoa
elimu huku ikiwataka wanaofika kwenye maonesho hayo kufika kwenye banda lao lililopo
katika Banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ili kupatiwa elimu
Alisema wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli
wanazofanya kwa kutumia Sheria ya Ushindani na Sheria ya Alama za bidhaa.
“Tuko hapa tangu Juni 28 mwaka huu
tukitoa elimu kwa wananchi ili waifahamu FCC na shughuli zake, tunapenda
kushukuru kwa muitikio mkubwa ambao umejitokeza kuja kupata elimu, kuielewa FCC
na kujua inafanya nini kwa kupitia sheria zake mbili kwa maana ya Sheria ya
Ushindani na ile Sheria ya Alama za bidhaa.
“Karibuni muweze kuendelea
kujifunza FCC tunafanya nini katika upande mzima wa kudhibiti bidhaa bandia,
tunafanya nini katika suala zima la ushindani, tunafanya nini katika kuwezesha
biashara na uwekezaji,”amesema
FCC kama taasisi wezeshi wanasaidia watu wenye mitaji yao
ikiwamo wafanyabiashara wakubwa wanaotaka kuwekeza nchini.
“Pia kama mteja ana biashara yake amesajili nembo yake italindwa na
FCC, lakini kama kuna kampuni yake anafikiria haifanyi vizuri na angependa
kujiunga na kampuni nyingine FCC iko tayari kwa ajili ya kuichunguza na
kuangalia kama muunganiko huo hauna madhara katika ushindani,”
“Kama kuna biashara unafanya
katika soko lakini kuna mshindani mwenzako anakufanyia miendeno isiyokubalika
kwa mujibu wa sheria, FCC iko tayari kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kutoa
adhabu iwapo mfanyabiashara atabainika anakinzana na sheria ya ushindani.
“Kwa hiyo tuko hapa kwa ajili ya
kuwezesha biashara, tuko hapa kwa ajili ya kulinda biashara lakini tuko kwa
ajili ya kumlinda mtumiaji.
Naye Afisa uchunguzi wa FCC alisema Sheria ya Ushindani namba
Nane ya mwaka 2003 inakataza mambo makubwa matatu. Moja ni makubaliano baina ya
washindani yanayokiuka ushindani.
“Baadhi ya mambo hayo ni kama makubaliano baina ya washindani
kupanga bei, washindani kupunguza uzalishaji au usambazaji wa bidhaa au huduma
lakini pia inakataza makubaliano baina ya washindani kupanga njama kwenye zabuni
“Jambo la pili ambalo linakatwaza na Sheria ya Ushindani ni
matumizi mabaya ya nguvu ya soko kuwa na nguvu ya soko sokoni kwa
wafanyabiashara ni jambo jema na ni ishara ya kuimarika kwa biashara lakini
namna nguvu hiyo inavyotumika inaweza ikasababisha uvunjifu wa sheria ya
ushindani.
“Kwa mfano pale ambapo mfanyabiashara mwenye nvuvu sokoni
akawa anatumia nguvu hiyo kukataa kutoa huduma au bidhaa kwenye baadhi ya sehemu
au kwa baadhi wafanyabiashara, hilo ni kosa kwa mujibu sheria ushindani namba
Nane.
Lakin mfanyabishara mwenye nguvu sokoni anazuiliwa na sheria
ya ushindani kutumia nguvu yake hiyo pale,”amesema.
Aidha ametoa mfano akiwa yeye ndio msambazaji au muuzaji wa
malighafi ambayo inatumika kutengeneza bidhaa fulani halafu akawa anawanyima
malighafi hiyo kwenda kutengeneza bidhaa hilo ni kosa kwani atakuwa anatumia
nguvu yake vibaya, nguvu ya soko vibaya.
Amesema lingine linalokatazwa na Sheria ya Ushindani ni
miungano ya kampuni ambazo zinatengeneza au kuimarisha hodhi ya soko, kwa
mujibu wa sheria ya ushindani inataka kampuni ambazo zinataka kuungana na
thamani yao inafikia bilioni 3.5 zinawajibika kutoa taarifa mbele ya FCC kabla
hazijaungana ili waweze kufanya uchambuzi wa kisheria na kiuchumi kuona kama
muungano huo au kununuana kwao hakutakuwa na madhara ya kisheria au kiuchumi
Wakati huo huo Afisa Kumlinda Mlaji katika Tume ya Ushindani
Amina Mjungu ameeleza jukumu mojawapo la tume hiyo ni kumlinda mlaji kuhusu
huduma na bidhaa anayoipata sokoni huku akifafanua mlaji ni mtumiaji wa mwisho
kabisa wa huduma na bidhaa.
“Katika kumlinda mlaji Tume ya Ushindani inapokea malalamiko
ya walaji na kuyapitia na kuyatatua ili kumaliza mgogoro husika.Pia inapokea
mikataba ya walaji inayoandaliwa na upande mmoja , mikataba ile inapitiwa
katika Tume ya Ushindani na kuhakikisha vile vigezo na masharti vinakidhi
viwango kwa pande zote za mlaji na mtoa huduma.
“Hivyo tunawahimiza watoa huduma walete mikataba yao ili
tuweze kuisajili katika Tume ya Ushindani kabla ya kutumika sokoni na watumiaji
sokoni ambao wamepatiwa huduma ambazo hazipendezi tume inapokea malalamiko yao
kupitia ofisi iliyopo Dar es Salaam au Dodoma.Pia wanaweza kuwasiliana nasi kwa
namba ya kupiga bure ni 0800110094.
No comments
Post a Comment