Vitendo vya uharifu ikiwemo Panyaroad vyakomeshwa katika mtaa wa Amani kata ya Kipunguni
Na Mussa Augustine.
Mtaa wa Amani Kata ya Kipunguni Jiji la Ilala Mkoani Dar es salaam,imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukomesha vitendo vya uharifu vilivyokua vikifanywa na baadhi ya makundi ya kiharifu ikiwemo kundi la Panyaroad.![]() |
| Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani Bw. Daniel Maragashimba wa kwanza kulia akiwa na Baadhi ya Wageni ambao ni wakazi wa Mtaa huo waliyokuja kumtembelea Ofisini kwake. |
Akizungumza na Mtandao wa Fullhabari Blog ofisini kwake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani Bw. Daniel Maragashimba amesema kwamba hatua hiyo inatokana na kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na jamii kushiriki ipasavyo katika kutoa taarifa za uharifu.
Aidha amesema kwamba Vijiwe Vyote Vya Bodaboda vimesajiliwa na kushirikishwa katika zoezi la Ulinzi shirikishi hali ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kukomesha uhalifu nakuifanya jamii Kufanya shughuli za maendeleo bila usumbufu wa aina yoyote.
" Hivi karibuni tuliitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla nakutoa maagizo kwa viongozi wote ngazi za mitaa kushirikiana kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi na Vijiwe vya Bodaboda vyote visajiliwe ili vishirikishwe kwenye Ulinzi shirikishi ,tayari tumetekeleza maagizo hayo na hali ya Usalama kwa sasa ni shwari " amesisitiza
Nakuongeza kwamba," hivi karibuni kijana anaesadikiwa ni Panyaroad ambaye alipora pikipiki akapigwa na Wananchi hadi kufa maeneo ya Tabata,hatua ambayo ilisababisha kundi la Panyaroad wenzake kumzika lakini ilikua shida katika maeneo mbalimbali kwani kundi hilo(Panyaroad) lilianza kuvamia Wananchi na kuwapiga hali iliyowalazimu baadhi ya Wananchi kufunga maduka yao,lakini nilishirikiana na viongozi wenzangu tukawakamata baadhi ya Vijana nasasa wapo kituo Cha Polisi Stakishari.
![]() |
| Muonekano wa nje wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Amani kata ya Kipunguni Jijini Dar es salaam. |
Kwa upande wake Polisi Kata wa kata ya Kipunguni Inspekta Msaidizi Fahamuel Nisaghurwe amebainisha kwamba mitaa ya Amani,Machimbo ,Kitinye na Kipunguni B, wamefanikiwa kuifanya kuwa tulivu kutokana na kuwepo kwa ushirikiano wa Polisi Jamii na Vikundi shirikishi.
"Kwa ujumla hali ya Usalama ipo shwari ,hivi vikundi shirikishi tunavipatia mafunzo ya muda ya namna ya kukabiliana na wahalifu,naomba kitumia fursa hii kuwaomba wadau wajitokeze kutusaidia mahitaji muhimu ikiwemo sare za rangi ya bluu kwa ajili ya Vijana wa Ulinzi shirikishi" amesema
Hahata hivyo Jaoel Lameck maarufu kama 'Chenga' ambaye ni Kamanda wa Ulinzi shirikishi mtaa wa Amani amesema wanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa posho za kujikimu wakati wanapotoka kwenye Ulinzi hivyo ameomba wadau kuchangia kiasi chochote kuwasaidia.
Hali kadhalika Charles Marwa maarufu kama "Klochi" ambaye ni Kamanda wa Bodaboda amedai kuwa changamoto kubwa kwao ni ukosefu wa vitendea kazi Kama vile makoti na tochi pamoja na posho za kujikimu hivyo ameomba jamii kujitokeza kuwasaidia ili waendeleee kukabiliana na vitendo vya uhalifu.


No comments
Post a Comment