NIDA wajipanga kuboresha vitambulisho vinavyokwisha muda wake
Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ( NIDA), Geofrey Tengeneza amesema wako mbioni kuanza zoezi la kuhuisha taarifa za vitambulisho vilivyotolewa mwaka 2012 ambavyo sasa vinaonekana vimepita muda wake
Aidha Tengenza aliwatoa hofu Watanzania juu ya kupata
usumbufu wa foleni kutokana na zoezi hilo linalotarajiwa kuanza hivi karibuni
kwani kitu kikubwa wanachoangalia ni upigaji wa picha, zoezi ambalo halichukui
muda mrefu.
“Vitambulisho vya Taifa vya mwaka 2012 vinaonesha kuisha
muda wake, watu hawatakiwi kuwa na hofu, tutavihuisha vitambulisho vyao, pia
alwataka kuendelea kutumia vitambulisho hivyo kwani utambulisho wao utabaki
palepale.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho
ya Biashara ya Kimataifa ya 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius
Nyerere, alisema kinachokwenda kuisha muda wa matumizi ni kibebeo cha
kitambulisho lakini utambulisho wa mwanachama unabaki palepale.
Alisema huduma zote ambazo wamekuwa wakizipata
kupitia kitambulisho hicho au namba ya kitambulisho utabaki kuwa palepale licha
ya muda wa kitambulisho kwenda kuisha.
"Licha ya kwenda kuisha kwa muda wa matumizi
ya kibebeo cha kitambulisho cha taifa naomba Wananchi mjue kuwa utambulisho wa
mwananchi unapaki pale pale na auishi muda wa matumizi"alisema
Tengeneza alisema kinachokwenda kufanyika baada ya
muda kuisha muda wa kitambulisho mwananchi atapaswa kwenda katika ofisi ya
wilaya katika eneo ambalo anaishi kufika pale kwa ajili ya kupigwa picha.
"Zoezi ambalo litafanyika ni kupiga picha tu
hakutakuwa na hatua uhakiki wa taarifa zako na baada ya hapo NIDA tutaendelea
utaratibu wa kuandaa kanzi data yetu"alisema
Aliendelea kufafanua kuwa matumizi ya kitambulisho
cha taifa yamekuwa ni ya miaka 10 lengo likiwa ni kufanya mabadiliko ya taarifa
za Wananchi tofauti na zile ambazo alitoa awali.
Akitaja sababu za kufanya mabadiliko ndani ya
miaka 10 Tengeneza alisema inawezekana mtu akawa amebadilisha makazi ya awali
hivyo ni lazima taarifa zake zikahuishwa katika mfumo wa kanzi data.
Pia alisema katika muda wa miaka 10 muonekano wa
mtu unaweza ukawa umebadilika hivyo katika kipindi hiki ni lazima afanye
mabadiliko.
"Hizi ndizo sababu ambazo kwanini tumeweka
muda wa miaka 10 nawaomba watanzania wasiwe na hofu yoyote Wala kuhusu foleni
pindi mchakato utakapoanza wa kupiga picha hakutakuwa na foleni ya aina yoyote
endapo hatakuwa na taarifa za kuhusisha"alisema
Vilevile alisema vitambulisho hivyo ambavyo ni vya
mwaka 2012 avitakuwa vikiisha muda mmoja na badala yake vinaisha kwa muda
tofauti kulingana na tarehe na mwezi na mwaka hivyo Wananchi wasiwe na hofu
kuhusu suala la foleni.
Aidha alisema NIDA imejipanga kutoa huduma hiyo
kwani tayari imekwisha toa oda ya vifaa vipya kwa ajili ya zoezi hilo.

No comments
Post a Comment