CDF Mabeyo akumbushia kifo cha Magufuli
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Jenerali Venance Mabeyo amesema katika kipindi alichokuwa kazini amekutana na changamoto kadhaa, ikiwamo kifo cha Rais John Magufuli.
CDF
Mabeyo alisema changamoto hiyo ilikuwa kubwa, lakini Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) lilisimama kidete kwa utulivu na kuhakikisha nchi inafuata
misingi ya katiba.
Kauli
hiyo kwa mara ya kwanza ameizungumza juzi usiku, katika mahojiano maalumu
aliyoyafanya kwenye kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha runinga
cha ITV.
“Ninyi
ni mashuhuda tukampoteza Rais aliyekuwapo madarakani, lakini tulisimama kidete
kwa utulivu mzuri kama jeshi tukitimiza wajibu wetu kwa mujibu wa Katiba,”
alisema CDF Mobeyo.
“Tukampokea
Rais Samia Suluhu Hassan na naamini tunaendelea vizuri mpaka sasa wananchi wako
watulivu wanaendelea kufuata miongozo kama inavyotolewa na Serikali.”
CDF
Mabeyo pia alizungumzia milima na mabonde katika safari yake ya uongozi wa
jeshi hilo, akisema hali hiyo ipo na itaendelea kuwepo kulingana na kipindi
kilichopo.
Katika
wakati wa uongozi wake kulikuwa na mazingira tofauti kwa kuwa matishio ya
usalama wa mipaka yanabadilika, hivyo ilikuwa changamoto kubwa.
“Nchi
yetu inakabiliwa na viashiria fulani vya ugaidi na ujue viashiria hivi vinaleta
matishio yasiyo na mipaka, adui haonekani waziwazi lakini tumeweza kushirikiana
na wananchi vizuri,” alisema CDF Mobeyo.
“Kama
mtakumbuka mwaka 2017 kulikuwa na mapango ya Amboni kule Tanga, baadaye ugaidi
ukazuka Mwanza, ikafuatiwa na Kibiti ambako ilikuwa ni kama kitovu, lakini
tukaendelea mpaka sasa tumehakikisha mpaka wetu upo vizuri.
“Ugaidi
mtu anaweza kutumika bila hata yeye kujijua, tunashukuru Watanzania wengi
wamekuwa wakishirikiana na Jeshi kutoa taarifa. Hatukuishia hapo tumeendelea
kuwa msaada kwa majirani zetu kuhakikisha tunalinda amani, hasa katika ukanda
huu wa SADC,” alisema.
Hata
hivyo, mkuu huyo wa majeshi alisema hali kwa sasa ni nzuri na Jeshi lina vikosi
ambavyo vimeendelea kulinda kwa kuwa baada ya kutoka Kibiti magaidi waliteremka
Kusini Mtwara.
Alisema
mpaka sasa hakuna changamoto ya kiusalama maeneo hayo na Jeshi limeendelea
kushughulikia usalama wa kikanda huku mipaka yetu ikiwa salama.
“Tanzania
ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na katika majukumu ni kuhakikisha dunia
inakuwa na amani, lazima tusaidie na tutaendelea kusaidia nchi nyingine katika
ulinzi wa amani, ni jukumu ambalo haliepukiki na tunapata manufaa kwa kujifunza
mambo mengi kitaaluma katika ustawi wa jamii, tunaneemeka mtu mmoja mmoja na
Taifa,” alisema CDF Mobeyo.
Hata
hivyo, alisema Tanzania haijawahi kuagiza wanajeshi waliokwenda kulinda amani
warejee mpaka watakapomaliza jukumu na kila wakipoteza wanajeshi wamekuwa
wakitoa taarifa kwa umma, “tukipoteza askari wetu huwa hatufichi, lazima taifa
lijue.”

No comments
Post a Comment