Sakata la mchakato wa mabadiriko ya katiba… LHRC wataka mabadiriko ya muundo wa Bunge Maalum la katiba
Mwandishi wetu
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
kimetoa maoni ya namna bora ya kuendelea na mchakato wa kupatikana kwa Katiba
Mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni
24, 2022 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Wakili Anna Henga
Ametaka kufanyika mabadiliko ya Sheria yote ya mabadiliko ya Katiba Na. 8/211
na kuweka muundo mpya wa Bunge Maalum la Katiba ili kuanza majadiliano na
kutunga Katiba Mpya.
“Bunge hilo litumie Rasimu ya Pili (II) ya
Katiba. Hii inatokana na ukweli kwamba, kulikuwa na mjadala mkali kuhusu
upatikanaji wa Katiba Pendekezwa, 2014,” amesema Wakili Henga.
Akizungumzia kuhusu faida ya njia hiyo,
amesema kwamba endapo Bunge Maalum la Katiba litaundwa kwa kuweka uwakilishi
mpana wa wananchi zaidi ya wabunge kutarudisha imani ya wananchi juu ya
mchakato wa katiba na kuwapa uhakika kuwa, masuala ya wananchi yanazingatiwa
vyema tofauti na kutanguliza zaidi maslahi ya baadhi ya wanasiasa.
Pia, amesema njia hii itajenga maridhiano na
kupunguza tofauti zilizopo kati ya wananchi na viongozi wa siasa.
“Aidha ni muhimu kukumbuka kuwa mchakato
wowote wa kufanya mabadiliko ya katiba ni lazima kuwepo kwa uhuru wa wananchi
kushiriki, kuafikiana na kumiliki mchakato wa kuandika katiba, kwani Katiba
inapaswa kutokana na ushiriki mkubwa wa wananchi,” ameongeza Wakili Henga.
Hivyo Wakili Henga ametoa wito kwa Serikali
Kupeleka muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili kuunda
upya Bunge Maalum likiwa na uwakilishi tofauti na wajumbe tofauti na wabunge
wachache wa vyama vyote wanaoweza kuwakilishwa.
Vile vile Serikali ipeleke mswada wa
mabadiliko ya Sheria ya Kura ya Maoni ili kuipa uhalali wa kisheria sheria hii.
Aisha Bunge Maalum la Katiba litakaloundwa
litumie Rasimu ya Pili (II) ya Katiba katika majadiliano yake.
Kadhalika Serikali iendelee kufungua milango ya majadiliano miongoni mwa watanzania kwa njia ya mikutano, makongamano, midahalo na vyombo vya habari juu ya mambo ya msingi na muhimu ndani ya katiba kwa mstakabari wa taifa letu.

No comments
Post a Comment