Zinazobamba

KIDATO CHA NNE ST. MATTHEWS WAWEKA REKODI YA UFAULU

MALENGO matatu yaliyowekwa na uongozi wa shule ya sekondari  St.Mathew's iliyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani,Malengo hayo yamezaa matunda ambapo wanafunzi wote waliomaliza  kidato cha nne mwaka 2021 wamefauku kwa kishindo katika matokeo yao.

Malengo matatu yaliyowekwa na shule hiyo kwa kila mtoto ni elimu, usalama na malezi.

Katika kuhakikisha wanafunzi wanafanya vyema katika masomo hayo,walimu walijikita kusimamia,malezi,usalama na elimu ambapo Mambo hayo yamezaa matunda katika ufaulu.

Akitangaza matokeo ya kidato cha nne,ya mtihani wa mwaka jana 2021,Katibu  Mtendaji wa Baraza la mitihani,shule ya sekondari st.Mathew's.  ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri mitihani yake ya kidato Cha nne mwaka 2021..

Wanafunzi wote waliomaliza katika shule hiyo wamefaulu kwa kishindo ambapo Kati ya wanafunzi 85 30 wamepata daraja la kwanza,45 daraja la pili na 15 ndio wamepata daraja la tatu.,huku  kukiwa hakuna  mwanafunzi aliyepata daraja la nne au kupata daraja la mwisho yaani ziro.

Ufaulu huo unaifanya shule  kuwa miongoni  mwa shule zilizoongoza katika ufaulu  wa matokeo hayo kuanzia ngazi ya Wilaya,Mkoa na taifa.

Matokeo hayo yanafanya wanafunzi wote waliofanya mtihani St. Matthews kuwa miongoni mwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu kitaifa ambao wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka daraja la tatu ikiwa ni asilimia 35.84 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani wa taifa kidato cha nne mwaka 2021. 

Akiongea kwa njia ya simu mkuu wa shule amewapongeza wanafunzi wote waliofanya mtihani huo kwa matokeo mazuri, na amewashukuru walimu wote, wazazi na walezi kwa ushirikiano mkubwa na jitihada walizoweka kuhakikisha watoto wanasoma vizuri. Shule imeahidi kuendelea kusimamia malengo yao matatu kwa kila mtoto, ambayo ni Elimu, Malezi na Usalama.

Hongera kwa shule kwa ufaulu mzuri, hongera kwa wanafunzi, wazazi, walezi, na walimu.

Nae mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo,Peter Mutembei ,ametoa  pongezi kwa wazazi, walimu, wahitimu na walezi.

Anasema misingi mitatu waliojiwekea katika shule imezaa matunda na itaendelea kuzaa matunda.

Anasema misingi hiyo imetumika katika elimu ya msingi na awali ya katika shule ya st. Mathew's ambapo wanafunzi waliomaliza darasa la Saba mwaka Jana wote walifaulu kwa kupata daraja A na kufanya shule hiyo kushika nafasi ya kwanza  kiwiliya na kufanya vizuri katika kimkoa na kitaifa.
Baadhi ya matokea ya wanafunzi wa shule ya ST. Mattews

No comments