Ubungo Islamic: Shule kongwe iliyobaki jina tu!
Ubungo Islamic ni shule kongwe ya Kiislamu ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1992, lengo lake likiwa ni kuwaelimisha vijana wote wa Kiislamu, bara na visiwani, kuwaandaa na kuwajenga vijana kiroho na kimwili kuondokana na ujinga, kutambua Mungu wao na kuwa viongozi waadilifu watakaotetea haki za wananchi na kutatatua matatizo ya jamii inayowazunguka, lakini pia imejidhatiti kutoa elimu ya mazingira katika Nyanja zote kwa kiwango cha hali ya juu.
Shule ya Ubungo Islamic imekuwa mstari wa mbele kuwaanda vijana wa kiislamu kuzikabili changamoto za mifumo mbalimbali duniani pasi na kupoteza itikadi sahihi ya kiislamu.
Shule
ina mazingira mazuri ya kukua kwa watoto, inamazingira ya kisomo na kimalezi
kwa ajili ya ulezi na kusoma, kwa muda mrefu imekuwa ni shule ya jina kubwa
katika uso wa Tanzania, inajamii kubwa ambayo imewahi kupita hapa, kwa upande
wa walimu shule ina walimu wenye sifa na uzoefu wa kutosha kazini.
Huduma
kubwa inayotolewa hapa ni hiyo elimu, tunao wanafunzi wa kuanzia kidado cha
kwanza hadi cha sita, lakini pia tunao wa shule ya awali (chekechea).
Kuanza kwake…
Wazo
la kuja na shule ya Ubungo Islamic limetoka mbali, shule ilianza kama madras
miaka ile ya 90, baadae ikaja fikra ya kuanzishwa kwa masomo ya sekula, Alhamdullah
wazo hilo lilifanyiwa kazi, toka ianze kutoa elimu ya dini na mazingira shule
ina umri wa takribani miaka 27.
Swali:
Wewe ni mdau mkuu katika shule hii, msomaji angependa kufahamu ufaulu ukoje
ukilinganisha na miaka mingine? Jitihada za kuondoa daraja sifuli na la nne
zimefikia wapi?
Jibu:
ni swali zuri sana ndugu mwandishi wa habari, tokea kuanzishwa kwa shule hii
tayari wameshapita wakuu wa shule 6, wote kwa wakati wao walipambana kuhakikihs
ashule inafanya vizuri,
Wamekuwa
wanafnya hivyo bila kuchoka, utakubaliana na mimi kuwa miaka ya nyuma, shule
imekuwa ikifanya vizuri sana, lakini taratibu jina lake limekuwa likififia
katika masikio ya waislamu, nitakuwaambia kwa nini, lakini elewa kuwa Ubungo
Islamic ni ileile, jana leo hadi kesho,
Takribani
wakuu wa shule sita wameshapita shuleni hapa, kila mmoja kwa jitihada zake
alikuwa anapambana kuhakikisha shule inakuwa na ufaulu mzuri, kuhakikisha
inakuwa kimbilio la waislamu wengi, jitihada hizo zimekuwa zikizaa matunda
taratibu.
Mfano
katika miaka sita ya hivi karibuni (2014-2020) , licha ya kwamba utaratibu wa
kuwadahili wananfunzi kwa njia ya kuwachuja ulibadilika na kuja na mfumo wa
kudahili wanafunzi kulingana na uwezo wao wa kifedha, yaani kumudu kulipa ada,
tumeweza kufanikiwa kufuta kabisa daraja la sifuli na la nne kwa wanafunzi wa
kidato cha sita.
Ni
mafanikio makubwa ambayo naweza kujifaharisha nayo kwa sababu haikuwa kazi
rahisi kufika hapo.
Zamani
Ubungo Islamic ilikuwa ni shule ambayo inakimbiliwa na wengi na ilikuwa na
ufaulu mkubwa, kilichokuja kuharaibu ufaulu wa shule ni kubadilika kwa sera,
tualiacha sera yetu mama ya kuchukua wanafunzi wenye ufaulu mzuri katika
mitihani yao ya mwisho, tuliacha sera yetu ya kuwachuja wanafunzi kabala ya
kujiunga na shule, shida ilianzia hapo, zamanimwanafunzi hawezi kuingia hivihivi,
ilikuwa ni lazima afike alama 41 (cut of point 41) ndio aweze kuchaguliwa
kujiunga na Ubungo Islamic, toka kuondolewa kwa mfumo huo mambo yamebadilika
kabisa.
Shule
sasa imekuwa ikipata watoto wenye uwezo hafifu, kazi imekuwa kubwa Zaidi, yaani
walimu wanakuwa na kazi kubwa ya ziada kuwarekebisha ili wawe na uwezo wa
kukabiliana na mitihani.
Licha
ya kwamba tunayo hiyo changamoto, kama shule tumekuwa tukijitahidi hivyohivyo,
tumeweka malengo angalau tufute daraja sifuri na kuondoa daraja la nne,
tumekuwa tukifanya hivyo na hakika kuna mwanga tunauona.
Mikakati yetu ni kuhakikisha kuwa haturudi
tena kwenye daraja la nne, tunaishia daraja la kwanza, pili na tatu.
Swali:
Ni upi mchango wa wanafunzi wanaopita hapa, (Alumn)
Jibu:
Sisi tunavijana wengi ambao wametawanyika katika Taasisi mbalimbali, naweza
sema hakuna Taasisi yoyote hapa nchini ambayo haina kijana wetu, iwe ya binafsi
au serikali, kifupi tumeenea nchi nzima, hiyo ni kwa sababu ya ukongwe wetu,
tuna utaratibu wa kukutana nao kila mwaka na kuwaeleza/kuwakumbusha juu ya
uadilifu, na wao pia wanatupa uzoefu wao huko makazini, uhusiano huo na
wanafunzi wetu unatupa faraja sana.
Swali: Unaona changamoto gani katika sekta hii
ya elimu, kwa sasa
Jibu:
Naona kama changamoto tatu hivi kwa harakaharaka, sekta ya elimu ni pana na
inashikiliwa na upande wa walimu, wazazi, wanafunzi na uongozi, kwa mfano hapa
Ubungo Islamic tatizo kubwa ambalo tunalo ni aina ya vijana tunao wapata
shuleni, walimu wanaoletwa bado wadogo pamoja na gharama za uendeshaji wa
shule,
Nikianza
na changamoto ya watoto, vijana wengi wanaoletwa ni wadogo sana, ni kama
wanakuja kukua, motto anafika hajui hata umuhimu way eye kwenda shule sasa
mzigo wote wa kuhimiza mtoto unakuwa kwa mwalimu na mzazi, tunafanya kazi ya kulea
watoto kimaadili, saiklojia ili tuwafanye wapende shule.
Kwa
upande wa walimu pia kuna changamoto, walimu wengi wanaoletwa umri wao bado ni
mdogo, unaona kabisa kunakipindi ambacho anapitia hivyo unahitaji kumlea
kimaadili ili asiharibu watoto wetu, kama unavyofahamu kuwa hapa tunao pia
wanafunzi wa kike, tunayo kazi kubwa za kuwarekebisha tabia zao.
Changamoto
ya kifedha, nafahamu kuwa shule nyngi za kiislamu zinachangamoto ya mitaji,
unajua hata katika shule ambazo zinafanya vizuri na kusifiwa ukiangalia
mazingira yao unaona kabisa ni watu ambao wamejitoa, wamewekeza fedha nyingi
sana
Wana
kila kitu, wana walimu wazuri, wanafunzi wazuri lakini pia miundo mbinu mizuri,
ni rahisi hata walimu kupanga program kulingana na mahitaji,
Kwa
upande wa shule za kiislamu naona kama hiyo ni changamoto, mfano ni hapa Ubungo
Islamic, tatizo hilo linaathiri sana utendaji wa shule, mwalimu mkuu kama kocha
katika timu anakuwa na wachaezaji wake ambao anaamini anamaliza nao msimu,
lakini ghafla wale wachezaji wazuri wanajikuta wanaondoka kwa sabbau ya fedha,
kwa hiyo program nzima inaharibika na anayeathirika ni motto pamoja na shule
yenyewe.
Unakuta
hamuwezi kumaliza mwaka tayari matatizo ya kifedha yanaikabili shule, hiyo ni
kwa sababu tunategemea ada za watoto. Imefikia wakati mfanyakazi ambaye uko
naye leo huna uhakika wa kesho kama atakuwepo, hakuna uhakika wa ajira,
Walimu
wazuri wote hapa wanakuwa kama wamejishikiza, wakipata sehehmu yenye donge nono
unakuta wanakiacha kituo na kukimbilia kwenye maslahi makubwa, haya mambo yote
ni kwa sbabau ya kukosa mtaji mkubwa kama wanavyofanya wengine.
Tunafukuzana
sana tu hapa shuleni, serikalini wakitangaza ajira unakuta walimu wote
wanakimbilia huko kwenye usalama wa ajira yao, shule inajikuta inaanza na moja
kutafuta walimu, mwalimu anayekuja hawezi kufanana na yule aliyeondoka, hapo
inakuwa changamoto kwa mtoto.
Kulegalega kwa shule…
Swali:
Ubungo Islamic inaoneka kuendelea
kupoteza umaarufu wake wa awali, yaani inalegalega na haina nguvu tena kama
zamani, unadhani tatizo liko wapi hasa?
Jibu:
Unachosema sio kweli, nitakupa sababu, machoni kwa watu wanadhani shule
imepoteza makali yake, lakini je ni kweli imepoteza makali au ni propaganda za
kibiashara?
Tukiangalia
takwimu zetu, shule yetu bado ipo katika mstari mzuri, bado tuko imara, sasa
hiyo hoja ya kwamba shule inashuka imetoka wapi, au wanafuata vigezo gani? Nitaka nikuhakikishie kuwa shule yetu bado
iko vizuri kwa mujibu wa takwimu zetu.
Ukiangalia
takwimu za shule zinatuambia ufaulu haujawahi kushuka sana, grafu inaonyesha
zigzag stlyle, yaani hakuna kupanda sana wala kushuka sana tupo katikati, sasa
kwa takwimu hizo unawezaje kusema kwamba shule imeshuka? Kinachoonekana hapo ni
mambo ya kibiashara, ili upate soko ni lazima utumie mbinu ya kupata wateja,
sasa wapinzani wetu sokoni wanatufanyia hayo, wanaeneza propaganda chafu kwa
watu ili tuonekane hatufanyi vizuri lakini nataka kukwambia hapa sisi
tunaendelea vizuri licha ya changamoto zilizopo.
Kadharika,
nakubali kukosolewa, najua ili kitu kizuri kitokee lazima tuangalie mapungufu
yetu ya ndani, sisi sio malaika inawezekana kabisa tunazo changamoto zetu za
ndani zinazotufanya watu watuseme vibaya, hakuna haja ya kujisifu wenyewe, kama
hilo lipo kama unavyouliza nadhani tutalifanyia kazi,
Tunaweza
kujiangalia wenyewe ndani tumejikwaa wapi hadi shule imekuwa haivumi kama
zamani, tusiwe watu wa kujivunia ukongwe wetu bila kujitathmini, kusemwa kwetu
kwamba tunapoteza mvuto tuliokuwa nao tusichukie hata kidogo, tuichukue hiyo
kama changamoto tufanye mabadiriko ili tusonge mbele.
Athari kutokana na kupoteza mvuto…
Kwa
kweli tunapata athari kubwa kwa kwa kupoteza mvuto, kwa mfano idadi ya
wananfunzi wanaojiunga na shule yetu imeendelea kushuka mwaka hadi mwaka, mwaka
2016 wanafunzi ambao walijiunga na shule yetu walikuwa 200, mwaka uliofuata
walishuka hadi kufikia 130, mwaka 2018 ndio ukawa mbaya zaidi, wanafunzi 50
pekee ndio tuliweza kuwasajili, takwimu hizi zinakuonyesha ukubwa wa tatizo.
Tatizo
letu tunadhani kwamba bado tunaeleweka kwa jamii kumbe mambo yamebadilika, hivi
sasa kuna shule nyingi za Kiislamu, watu wanatumia matangazo mbalimbali
kuwavutia wateja, ni ulimwengu wa mashindano, sisi bado tumejisahau, huwezi
kutusikia popote tukitangaza huduma zetu, mara nyingi tumekuwa tukitumia gazetu
letu la Taasisi, lakini bado mambo si mazuri.
Kujikwamua
na changamoto hizi nadhani tunahaja ya kuingia katika ushindani, tutangaze
bidhaa zetu na watu watufahamu kwamba tumerudi kwa ujio mpya, lazima turudi
katika nafasi yetu.
Karne
ya sasa imekuwa na ushindani mkubwa, miaka ya nyuma tulikuwa tunasikika sana
kwa sababu kulikuwa hakuna ushindani, shule pekee iliyokuwa ikitegemewa na
waislamu ni Ilala Islamic, lakini leo hii kuna shule nyingi tena zenye
uwekezaji wa kuridhisha. Kwa hiyo hata mvuto wetu umepotezwa na ushindani pia.
Enzi
hizo kulikuwa hakuna wapinzani katika sekta hiyo ukiachana na Masjid Quba, na
kwa mantiki hiyo Ubungo Islamic ilikuwa inachagua nani aingie na nani asiingie,
kwa sababu Waislamu wote walikuwa wanaiangalia shule kwa jicho la kipekee, kila
Muislamu alikuwa anatamani mtoto wake asome
Ilikuwa
ni lazima mwanafunzi afikishe alama 41, mwanafunzi kama hujafikisha alama hizo
huwezi kuingia hata iweje, hali hiyo ilikwenda hivyo kwa miaka mingi,
Zimekuja
shule mpya za kiislamu zikachukua na sera yetu ya kuchuja, wanaweza kufanya
hivyo kwa sababu hawategemei ada za
wanafunzi, sisi tumejisahau, tumekuwa tukiendesha shule kwa mifumo ya zamani,
wenzetu wamekuja na mifumo tofauti, unakuta wanamiradi mbalimbali inayowafanya
waweze kuendesha shule, ada inakuwa tu sehemu ya kuboresha miundo mbinu lakini
haitegemei sana kuendesha shule, ndio maana wanauwezo wa kukataa wanafunzi
ambao hawafiki vigezo vyao licha ya kwamba wanafedha za kulipa ada.
Migogoro
ya kiongozi, hii inaua shule, hapa nishauri hasa kwa shule zetu za kiislamu,
zisiendekeze migogoro, chuki na visasi, vitu hivyo vinaweza kuua shule, hiyo
naina kama changamoto katika uongozi, mfano utawala ukipita basi watoe fursa ya
utawala mpya kufanya kazi kwa kujinafasi, wasianze kufanya chokochoko
ikapelekea kazi kuwa nzito,
Lakini
pia wawe tayari kukubali kuachia nyadhifa zao bila chuki, wasianze kusambaza
maneno kwa umma kiasi ambacho unaathiri taasisi ambayo ulikuwa unafanyia kazi,
nimeliona hilo nikabidi nitoe ushauri wangu hapa.
Unakuta
kila kiongozi ambaye amepita katika shule flani akaanza kuissema vibaya shule kwa
watu wake wanaomuamini inaleta picha gani kwa jamii, huko ni kuichafua shule.
Kuna
baadhi ya viongozi hatujaachana nao vizuri, wengine wamefukuzwa, sasa wanasema
vibaya shule na wanaiumiza kwa vitendo vyao hivyo. Tumedumu katika hali hiyo
kwa muda mrefu.
Tunaweza
tukatoka, lazima tukubali mabadiliko vinginevyo hatuwezi tukatoka, tukubali
kuwa sasa hivi shule iwe sehemu ya biashara, maana yake lazima tuitangaze, na
kuitangaza lazima tutangaze huduma bora zinazotolewa hapa, ukitangaza huduma
laikini watu hawaoni ubora huo watu bado watakukimbia, lazima turudi tujipange
upya, tutengeneze huduma zetu na tuzitangaze, shule hii huwezi isikia
ikitangazwa sehemu yeyote ile mbali na gazeti la Taasisi, tutoke huko,
tujifunze hata kwa wenzetu waliofanikiwa, tusiamini kwamba watu wanaifahamu
shule.
Lingine
tuwe na utamaduni wa kuwapa uhakika wa kazi kwa walimu wetu, leo we umenikuta
hapa kesho huwenda sipo…tunafukuzana sana hapa kwa sababu ndogondogo sana,
walimu wengi hapa wana hofu, hawajui kesho yao watakuwa wapi, unakuta mwalimu
uliyeanza naye juzi leo hauko naye, shule inakuwa inaanza moja kila kukicha,
tusiwafanyie hivyo walimu, tuwatendee haki (treat them fairly)
Umuhimu wa kuwaamini wale uliowapa madaraka
Katika
jambo ambalo linanikera ni kukosa nguvu ya maamuzi katika sehemu yangu ya kazi,
ili shule iende inahitaji watumishi wake wafuate muundo wa uongozi, lakini
linapokuja suala la kuingiliana katika majukumu inakuwa ni changamoto kubwa,
mtumishi anakosa kujiamini hali inayopelekea ufanisi wake kupungua.
Prepareb
by MAGALI
SOURCE: Mkuu
wa Shule Ubungo Islamic, Hudhaifa Abdulmaliki Khouf
Hakuna maoni
Chapisha Maoni