Maren Montovani: Wapalestina wanastahili huruma
Mwenyekiti wa Kamati ya mshikamano wa Tanzania na Palestina Abdallah Miraj Othman |
Mwanaharaki na msomi wa hali ya juu kutoka nchini Italia anayepigania haki za Wapalestina Bi. Maren Montovani akizungumza na Waandishi wa habari |
Katibu wa Kamati ya mshikamano wa Tanzania na Palestina, Nizar Visram |
Mwandishi wetu
Mwanaharaki na msomi wa hali ya juu kutoka nchini Italia anayepigania haki za Wapalestina Bi. Maren Montovani amewashauri watanzania kuendelea kupaza sauti ili wapalestina wapate ukombozi wa kweli.
Bi Maren ambaye amefika nchini Novemba 30, 2021 akitokea nchini Msumbiji alikoenda kuzungumzia hali ya Palestina amesema kwa sasa wapalestina wanaishi kwa mateso nchini mwao.
Amesema wapalestina wananyanyasika kwa kuvamiwa, kupiga na hata makazi yao kubomolewa jambo ambalo si haki hata kidogo.
Mtaalamu huyo ambaye ametumia muda mwingi kuonyesha picha kadhaa kwa waandishi wa habri zinazoonyesha ukatili wanaofannyiwa wapalestina amesema hali ni mbaya na kila mwenye huruma anapaswa kupaza sauti.
KAMATI ya mshikamano wa Tanzania na Palestina imetoa rai kwa
watanzania kuendelea kupaza sauti zao ili kuvifanya vyombo vya kimataifa kuchukua
maamuzi sahihi ya kuwasaidia wapalestina kupata haki yao ya msingi ikiwamo haki
ya kuishi katika taifa hilo bila kubughudhiwa.
Aidha wametaka Tanzania kama nchi ambayo inahistoria kubwa katika
masuala ya harakati za ukombozi wa mataifa ya Afrika na nje ya Afrika
wajitahidi kudumisha utamaduni huo wa kusaidia wengine pindi wanapoona
wanaonewa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya
mshikamano wa Tanzania na Palestina Abdallah Miraj Othman amesema inauma sana
kuona kuna taifa hapa duniani bado linapambana kupata uhuru wake huku mataifa
mengine yakiwa hayatoi kipaumbele cha kuwasaidia kwa haraka.
“Tunatoa wito kwa watanzania tupaze sauti zetu kuwasemea ndugu
zetu wapalestina, miaka ya nyuma tulikuwa mbele katika kuwasemea Palestina,
hivi sasa tumeshuka katika kupaza sauti zetu,” alisema Miraji.
Kuna propaganda nyingi zimeingizwa hapa Tanzania kuhusu suala hili
dhamira ikiwa watanzania waache kupaza sauti juu ya kupinga vitendo Aidha amesikitishwa
kuona kuna baadhi ya watu wanalichukulia suala la Palestina kama ni jambo la
kidini na kusisitiza kuwa jambo hilo
halijakaa kidini japo ni kweli kuna kunabaadhi ya watu wamelivarisha vazi la
kidini suala hilo ili watu wengine wasiwasaidie Wapalestina.
“Suala la Palestina halina uhusiano na dini, ni suala ambalo
linazungumzia haki ya watu kuporwa ardhi yao, kama tulivyokuwa tunaipigania haki
za Wasauzi Africa, Namibia Msumbiji na nchi
zingine za Afrika ni sawasawa na kupigania suala la Palestina, tunachotakiwa
kufanya ni kupaza sauti zetu,” aliongeza.
Akizungumzia hatua iliyochukuliwa na serikali ya Tanzania juu ya
kupinga Izraeli kupewa siti katika umoja wa Afrika, Miraji amesifu hatua hiyo
na kuonyesha kuwa Tanzania bado tunao msimamo uleule ulianzishwa na baba wa
taifa wa kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya Wapalestina.
“Kama kamati tunaunga mkono msimamo wa serikali ya sita inayoongozwa
na mama Samia Suluhu Hassani, yenyewe inaunga mkono juhudi za kuwafanya
waisraeli na wapalestina kuishi kwa amani ni jambo kubwa na tunalolitamani
kutokea,” alisema.
Amesema sio haki hata kidogo kuona kundi moja linakandamizwa,
kunyanyaswa na lingine likifurahi na kucheza kwa amani.
Akizungumiza kasi ya wapalestina kupotea katika ardhi yao, amesema
kasi hiyo ni kubwa ambapo mpaka sasa Takwimu zinaonyesha waisraeli
washajimilikisha eneno kubwa ukilinganisha na wengine.
“Katika miaka ya 1947 ardhi ya Palestina, ilikuwa inakaliwa na wapalsetina wenyewe kwa
asilimia 80, lakini hadi inafika mwaka 2021, ardhi ya hiyo imeshachukuliwa na
waislael asilimia 80, kibaya Zaidi hata asilimia chache iliyobakiwa bado bado
haina amani, wamekuwa wakafanyiwa ukatili wa kila aina,” alifafanua
Amesema Wapalestina wamekuwa hawana amani, wanavamiwa katika
makazi yao, wanavunjiwa, wanateswa lakini kubwa Zaidi wanauliwa, mambo haya
yanatia uchungu sana na kushauri watanzania kuungana kupaza sauti ili mambo yaweze
kuzuiliwa.
Naye Katibu wa Kamati ya mshikamano wa Tanzania na Palestina,
Nizar Visram amesema suala la Palestina ni Suala la ukombozi hivyo kamwe
lisinasibishwe na masuala ya kidini.
Amesema ubaguzi wa rangi uliopo Afrika Kusini ni ubaguzi uleule
unaoendelea nchini Palestina kwa sasa, Tanzania inayo historia nzuri ya kuunga
mkono harakati za ukombozi katika Afrika na Nje ya Afrika, pia tumekuwa
tukiunga mkono harakati za Palestina, ni msimamo wetu.
“Nataka niwaambie, ni kweli dunia inabadirika lakini msimamo wa
Tanzania haujabadilika, bado tunaunga mkono hrakati za ukombozi za Palestina,
Mama MuraMura amethibitisha hilo kwa vitendo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni