Wachimbaji wadogo wa madini sasa kupatiwa mikopo isiyo na riba, STAMICO, KCB waingia makubaliano
Mwakilishi wa Benki ya KCB, Mkuu wa Kitengo cha
Huduma za Kiislamu wa Benki hiyo (Islamic Banking) Amour Muro akizungumza
kwenye hafla hiyo. |
Mwandishi wetu
Wachimbaji
wadogo wa madini wana kila sababu ya kutabasamu kufuatia habari njema ya Shirika
la Madini la Taifa (STAMICO) na Benki ya KCB kuingia makubaliano yanayolenga
kushirikiana katika kutoa mikopo ya kuwawezesha kupata mikopo endelevu na kwa
rahisi zaidi ili waweze kufanya shughuli za uchimbaji zenye tija.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya STAMICO kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake, Dkt.
Vennance Mwasse amesema mikopo hiyo inategemewa kuleta tija kwa wajasiliamali
lakini pia kwa taifa.
“Mpaka
sasa wachimbaji wadogo wanaongoza kwa kupatiwa leseni ukizingatia na wadau
wengine, kimsingi unaposema wachimbaji
wadogo maana yake ni wazawa, hadi sasa leseni 34,000 zimeshatolewa, makubaliano
haya yatawasaidia watanzania kuleta tija katika biashara zao,” alisema Dkt
Mwasse
Makubaliano
hayo yamefikiwa baada ya kusaini Hati ya makubaliano (MOU) baina ya pande hizo
mbili Novemba 16, 2021 katika Ofisi za STAMICO Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa utiaji saini wa Makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
STAMICO Dkt. Vennance Mwasse amesema kuwa Malengo ya makubaliano hayo ni
kushirikiana na Taasisi za fedha katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata
mikopo endelevu na yenye tija.
"Katika
Makubaliano haya STAMICO itawajibika kutoa utaalam elekezi katika maeneo ya Jiolojia,
Uchimbaji na Uchenjuaji Madini kwa miradi ya Wachimbaji Wadogo ambayo itafanya
maombi ya mikopo na kuiwasilisha kwa Benki kabla ya utekelezaji wake na Benki
ya KCB itawajibika kutoa mikopo kwa Wachimbaji Wadogo ambao watawasilisha
maombi ya mikopo katika maeneo ya miradi ya uchimbaji madini itakayokidhi
vigezo vya kupewa mikopo.Amesema Dkt. Mwasse.
Ameongeza
kuwa Makubaliano hayo yatadumu kwa muda wa miaka mitatu (3) kuanzia mwaka huu
wa 2021 ambapo pia yanaweza kufanyiwa mapitio kila baada ya mwaka mmoja (1).
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Benki ya KCB, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kiislamu
(Islamic Banking) Amour Muro amesema wafanyabiashara ambao wanaogopa kukopa kwa
sababu ya riba sasa hawana cha kuogopa kwa sababu wako tayari kutoa mikopo hiyo
bila riba yeyote.
Aidha
amesema suala la riba halibagui dini, mfanya biashara yeyote anayetaka kukopa
bila kula ripa anachopaswa ni kusema na KCB wako tayari kuwahudumia.
Aidha
Mtaalamu huyo wa mambo ya fedha amesema ametoa wito kwa wachimbaji wadogo
waislam na wasio waislam kujitokeza kuchukua mikopo isiyo na riba.
"Mpaka
sasa Benki yetu tayari imeshatoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 4 kwa
wateja wetu wote na sasa tupo tayari kuwafikia wachimbaji wadogo kwa kuwakopesa
ili waweze kufanya shughuli zao" Amesema
Amour.
STAMICO
imendelea kutekeleza mikakati yake ya kuendeleza shughuli za uchimbaji mdogo
nchini ili uwe wenye tija na kuchangia ipasavyo uchumi wa nchi ikiwa ndio Mlezi
wa Wachimbaji Wadogo hapa nchini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni