Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuzuru Tanzania hivi karibuni
Waziri wa Nishati, January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Balozi Richard Kabonero.
Mazungumzo
hayo, yamefanyika Novemba 15, 2021 katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati
zilizopo jijini Dar es Saalam.
Katika
kikao hicho ambacho walijadili maandalizi ya ziara ya Rais wa Uganda, Yoweri
Museveni ambae anatarajiwa kuanza ziara nchini Tanzania hivi karibuni.
Aidha,
Makamba alisema kuwa Uhusiano mzuri uliopo baina hizo nchi hizi mbili
umepelekea kurahisisha ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika
Mashariki (EACOP) na Marais wa nchi hizo mbili watahakikisha kuwa mradi huo
unakamilika.
Pia,
alisema mradi wa EACOP ni muhimu sana katika nchi hizo mbili na mpaka sasa upo
kwenye hatua nzuri.
“Tunafurahi
hatua kubwa iliyofikiwa katika mradi na tunajua umuhimu wa mradi huu kwa nchi
zetu zote mbili,” alisisitiza
Waziri Makamba.
Kwa
upande wake, Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Balozi Richard Kabonero
ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano waliotoa kwa kuhakikisha mradi
wa Bomba la mafuta unafanikiwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni