Zinazobamba

TBS YATOA MAFUNZO YA UDHIBITI UBORA KWA WAJASIRIAMALI WA MAZIWA MKOANI PWANI

 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Sara Msafiri akifungua mafunzo kwa wajasiriamali wasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa maziwa na bidhaa za maziwa wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

   Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe Sara Msafiri (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo kwa wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa.

  Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa wilayani kibaha wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wametoa mafunzo ya Udhibiti ubora kwa wajasiriamali ambao niwasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa maziwa na bidhaa za maziwa mkoani Pwani.

Akizungumza na washiriki wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Sarah Msafiri alisema amefurahishwa sana na  uamuzi wa TBS  kuamua kutoa mafunzo kwa wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa na kuichagua wilaya ya Kibaha kuwa sehemu ya kwanza kabisa kupokea mafunzo hayo na nimatarajio yake kuwa wadau hawa watatumia vizuri fursa hii ya mafunzo ambayo itapelekea kuwa na uzalishaji wa maziwa na bidhaa za maziwa zitakazokidhi matakwa ya viwango.

Alisema anatambua nafasi walionayo  wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa katika kuchangia uchumi wa taifa hivyo basi kama watakuwa wasikivu katika mafunzo hayo mahususi kwa ajili yao ili kuwajengea uwezo na hatimaye kuwa bidhaa zitakazoweza kuuzwa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Bw. Hamisi S. Mwanasala mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu (TBS) alisema kuwa mafunzo haya yanafanyika  katika wilaya  Kihaha  na Bagamoyo ( Pwani) na Kilosa na Bagamoyo ( Morogoro) na yanatarajia kuwa endelevu kwa Tanzania nzima

Alifafanua kuwa mafunzo haya yatawanufaisha washiriki kwa kutambua faida na matakwa ya viwango vya maziwa na bidhaa za maziwa,  kanuni bora za usindikaji wa maziwa, kanuni bora za afya, teknolojia mbalimbali za usindikaji wa maziwa, utaratibu wa uthibitishaji ubora wa bidhaa, usajili wa majenngo ya kusindikia vyakula na kanuni bora za ufugaji.

Bw. Mwanasala alisema mafuzo hayo yamejumuisha wakufunzi kutoka taasisi mbalimbali kama vile TBS, SIDO, Bodi ya Maziwa , Afisa Biashara, Afisa Afya na Afisa maendeleo ya jamii.

Lengo la kutumia wakufunzi kutoka taasisi mbalimbali ni kuhakikisha kuwa mafunzo haya yanaleta tija kwa washiriki kwa kupata elimu juu ya taratibu na kanuni za uzalishaji bora wa maziwa na bidhaa za maziwa.

Hakuna maoni