Rais Samia Kutua Mwanza Kesho
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku
moja ya kikazi Novemba 18, mwaka huu kwa lengo la kuhudhuria maazimisho ya
Jubilee ya Miaka 50 ya Hospitali ya Bugando.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
Eng. Robert Gabriel amesema “Mhe. Rais Samia atakua na ziara ya kikazi mkoani
Mwanza ambapo atakuja kwenye maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya
Bugando”.
“Mhe. Rais anatarajia kuwasili
majira ya saa 12 Asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza kutokana na hali hiyo
ninawaomba wananchi wa Mkoa wa Mwanza wajitokeze kumkali pembezoni mwa barabara
mpaka atakapofika Rais wetu,” amesema Eng. Gabriel.
Hospitali ya kanda ya Bugando imebobea kutoa huduma bora za kibingwa na za kisasa
ambapo hospitali hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa kutoa huduma za kiafya kwa
wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa na hata nje ya nchi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni