Mtendaji mkuu NDC aanza na watendaji, awaasa waache mazoea
MKURUGENZI Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo NDC, Dkt Nicolaus Shombe akizungumza na watendaji wa shirika |
MKURUGENZI Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo NDC, Dkt Nicolaus Shombe akizungumza katika kikao hicho |
Na Suleiman
Magali
MKURUGENZI Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo NDC, Dkt
Nicolaus Shombe amewataka wafanyakazi kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala
yake wajikite katika kufanya kazi kwa viwango vya juu ili kulifanya shirika
kuwa la mfano.
Dkt Shombe ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuliongoza shirika hilo baada ya kifo cha Prof Damiani Gabagambi, amesema asingependa kuona watu wanafanya kazi kwa wanavyojisikia na kulipelekea shirika kushindwa kufikia ndoto zake za kutekeleza miradi kwa wakati.
Amesema anatamani kuona watu wanafanya kazi kwa juhudi na maarifa
ili kuhakikisha wanafikia ndoto ya kuwa shirika bora na la mfano kwa kutekeleza miradi mbalimbali
ya kimkakati ya serikali pamoja na kushirikiana
na sekta binafsi katika kukuza sekta ya viwanda hapa nchini.
Dkt Shombe ameyasema hayo mara baada ya kuwasili rasmi katika
ofisi za Makao Makuu ya NDC na kuanza kazi mara moja.
“Ninawaombeni sana ushirikiano wenu tukiwa
kama familia moja, tushirikiane pamoja katika kuhakikisha Shirika linasonga
mbele. Tukishirikiana tutaweza kuzitatua changamoto mbalimbali zinazotukabili,”
Alisema Dkt Shombe
nitahakikisha
tunatenga muda maalum ambao tutakuwa tunakutana na menejimenti,wakuu wa Idara pamoja
na wafanyakazi wote ili kusiwe na utofauti mkubwa baina ya viongozi pamoja na
watumishi wa kawaida lengo likiwa ni kujenga teamwork ” Alisema Dkt Shombe.
Dkt Shombe amehaidi kuzitendea kazi changamoto mbalimbali zilizo
ibuliwa na wafanya kazi huku akiwataka wafanyakazi kubainisha fursa wanazoziona
na mikakati ya kuzitumia kwa maendeleo ya viwanda nchini.
Kwa upande wake aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa NDC,ambaye kwa sasa
ni Mkurugenzi wa Fedha Rhobi Sattima alimpongeza
Dkt Shombe kwa kuaminiwa na Rais na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa
NDC huku akisema kuwa ana imani ataifanyia makubwa NDC.
“Mkurugenzi
ninakumbuka siku moja wakati uko Hazina kama Kamishina wa Mipango ulitusaidia
sana katika kuhakikisha kuwa taasisi inawezeshwa kifedha na nadhani ulifanyika kuwa
kama malaika kwani hatimaye leo umeteuliwa rasmi kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Shirika Hongera sana kwani tunamatumaini makubwa na ujio wako”Alisema Bi Rhobi Sattima.
Ujio wa Dkt Shombe kuwa Mkurugenzi mpya wa NDC umepokelewa vizuri
na wafanyakazi ambao wamehaidi kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha
anatimiza adhima ya shirika hilo.
Malengo ya shirika hilo ni pamoja na kuwa kinara katika ujenzi wa
Tanzania ya viwanda pamoja na kuvutia na kujenga mazingira bora wezeshi kwa
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Uteuzi wa Dkt Shombe kushika nafasi ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa
NDC na Rais umefanyika mara baada ya kufariki Dunia kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa
NDC Prof Damiani Gabagambi ambaye alifariki dunia Mwishoni mwa mwaka jana
ambapo kabla ya kuteuliwa na Rais kuwa mtendaji mkuu wa NDC Dkt Shombe alikuwa
anashika nafasi ya Kamishina wa Mipango ya Kitaifa kwenye Wizara ya Fedha na
Mipango.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni